Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu ametoa wito kwa, Taasisi mbalimbali
za serikali, kiraia na wadau mbalimbali wa maendeleo kuunganisha nguvu
dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto.
“Tumefanya tathimini kuhusu
hali halisi jinsi ilivyo kuhusu ukatili, changamoto bado zipo na tumekubaliana
tuunganishe jitihada, kwa kufanya kazi kama timu katika kupambana dhidi ya
ukatili wa wanawake na Watoto.”
Wito huo umetolewa katika
kikao cha dharura cha Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta wa Mpango wa Taifa wa
Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) kilichoongozwa na
Mwenyekiti Dkt, John Jingu Mjini Dodoma.
“Aidha tumekubaliana kuongeza
kasi ya utekelezaji katika maazimio mbalimbali ambayo tumekubaliana na jitihada
hizi tutaendelea kuzifanyia kazi na tathimini kila wakati ili kutokomeza
ukatili dhidi ya Watoto, alisema Dkt. Jingu”
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainabu Chaula amesema
tunapaswa kupaza sauti dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto kuanzia umri
usiojitambua mpaka umejitambua.
“Janga hili liko kwenye
ngazi ya kifamilia, tafiti zinaonyesha ukatili mwingi unaofanyika dhidi ya
watoto unazimwa katika ngazi ya kifamilia kwa sababu ya kuogopa kuleta migogoro.
Watoto hawa ambao hawana hatia unawasababishia kupata sonona, na utuuzima
usioeleweka, alisema Dkt. Chaula.”
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba na Sheria Bi, Mary Makondo amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya
mapitio ya sheria, sheria ya haki ya mtoto, sheria ya ndoa kwenye umri wa
mtoto na kuangalia wadau wote kwenye uendeshaji wa kesi.
Tunaamini kupitia wadau katika
huduma za msaada wa kisheria, tukienda pamoja kuwezesha huduma za msaada wa
kisheria lakini pia kutoa elimu ili kuona swala hili ni janga la kitaifa na
Watoto wanapaswa kulindwa.
“Mahakama kama muhimili
imekuwa ukitoa adhabu stahiki, lakini bado tunahitaji kuangalia mapitio ya
sheria za makossa ya jinai lakini pia mwenendo wa makossa ya jinai ili
kuhakikisha adhabu zinazotolewa zinaendana ili ziwe mafunzo kwa jamii katika
kuhakikisha haki za Watoto na wanawake zinalindwa alisema Katibu Mkuu Bi,
Makondo.”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.