Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi ameziasa Kamati za Maafa kuendelea kutoa elimu katika maeneo yao ili kujiandaa na kukabili maafa pindi yanapotokea na kuweka mkazo katika maafa yanayoathiri maeneo ya Wilaya hiyo.
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua semina ya siku 5 ya kujenga
uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii kwa wajumbe wa Kamati
za Maafa Wilaya hiyo iliyohusisha Kata sita zinazoathiriwa na maafa ikiwemo
Magoma, Foroforo, Kalalani, Dindira, Bungu na Kizara zilizopo Korogwe mkoani
Tanga.
Semina hiyo iliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IMO) imewafikia zaidi ya
wajumbe 50 kutoka katika Kata hizo ikiwemo Viongozi wa dini, Wazee Mashughuli
pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya aliwaasa wajumbe hao kuendeelea kuwa mabalozi
wazuri katika kutoa elimu juu ya kujikinga na madhara yatokanayo na maafa ili
kiuendelea kuwa na jamii iliyosalama
“Yatumieni mafunzo haya kama nyenzo muhimu katika maeneo yenu
kuhakikisha mnajilinda na maafa yanayoweza kujitiokeza katika maeneo yenu,
kukabili maafa kunahitaji kujitolea kwa mtu mmoja mmoja ili kuwa na mazingira
salama,”alisisitiza Mhe. Mwanukuzi
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya
Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Kanali Selestine Masalamado akieleza lengo la
semina hiyo ni kutoa elimu ya masuala ya maafa kuanzia ngazi ya Halmashauri
hadi Kijiji ikiwa ni moja ya jukumu la idara hiyo ili kuwa na uelewa mpana
kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa.
“Idara ya Menejimenti ya maafa imekuwa ikiendesha semina hizo
katika maeneo mbalimbali nchini ili kuendelea kuwajengea uelewa wananchi kuhusu
mzingo mzima wa menejimenti ya maafa unaohusisha kuzuia, kujiandaa kukabili,
kukabiliana, kurejesha hali pindi maafa yanapotokea katika maeneo yao,”alisema
Kanali Masalamado.
Aliongezea kuwa miongoni mwa maeneo yaliyofikiwa ni pamoja
na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa kuzingatia imekuwa ikikabiliwa na
maafa mbalimbali yakiwemo ya uhalibifu wa mazao unaosababishwa na uvamizi wa
wanyamapori(tembo), ukame, pamoja na mafuriko.
Naye Afisa Afya kutoka Wilaya ya Korogwe Bw. Majaliwa Tumaini
alieleza mada kuhusu ugonjwa wa ebola aliiasa jamii kuona umuhimu wa kujilinda
na kulinda wengine kwa kuzingatia madhara yatokanayo na ugonjwa huu.
“Lazima tuchukue tahadhari zote muhimu kwani ugonjwa huu upo
nchi jirani, kila mmoja awe mlinzi wa wenzake huku tukifuatilia maelekezo
yanayotolewa na Wizara husika na wataalam wa afya,” alieleza
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.