Wazazi wahimizwa kusimamia
misingi ya malezi kwa vijana wanapohitimu kidato cha nne kwa kuhakikisha vijana
hao wanaendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita ili kuendelea kuwafuatilia
kwa ukaribu mienendo ya tabia zao.
Wito huo umetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene
katika mahafali ya nane ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mtakatifu
Catherine iliyopo Lushoto Tanga.
Elimu hii inaushindani mkubwa
katika kazi, msome kwa ajili ya uelewa na msome kwa ajili ya kuja kushiriki
udahili katika ushindani wa kupata kazi na uwezo wa kujitegemea.
“Katika kipindi hiki ambacho
wanasubiria matokeo, wazazi msiwape uhuru vijana kwa sababu umri walionao bado
ni mdogo na bado wanahitaji malezi. Wekeni utaratibu wa kutumia simu janja
katika kipindi hiki ili waweze kuweka mkazo katika kutimiza malengo yao,”
alisema Waziri.
Sitegemei
kumwona mmoja wa wahitimu hawa akipotea katika maadili mabovu na matumizi ya
madawa ya kulevya bali ni matumaini yangu wote mtasonga mbele na kufikia ngazi
za juu kabisa za taaluma. Hii ni kwa manufaa yenu binafsi na taifa letu
kwasababu bado tuna uhitaji mkubwa wa wataalamu na ninyi ni sehemu ya wataalamu
tunaowahitaji hapo baadaye.
Naye Sr.
Fokas Mjema, Msaidizi wa Mama Mkuu wa Shirika la Masister wa Usambara
na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Catherine, amewashukuru walimu na
wanafunzi kwa kufanya mitihani ya majaribio kwa bidii na ungalifu na kuwa
makini.
“Wahitimu
wetu wa kidato cha nne wanafunzi 65; wameandaliwa vizuri, tunategemea kutokana
na maandalizi wapate ufaulu wa daraja la kwanza na ufaulu wa daraja la pili”
Akieleza
namna shule ya Mtakatifu Catherine ilivyojiaanda na Mtihani wa Taifa Mwalimu wa
Taalumu Nyandwi Mathias Marko amesema; shule inautaratibu wa kufanya mitihani
ya majaribio, mitihani ya majaribio kwa vitendo, mitihani ya mwaka, mitihani ya
kila wiki, mitihani ya ushirikano na shule nyingine na mazoezi.
“Tunatumia
mitihani hiyo kufanya tathimini kwa kuangalia udhaifu ili kuwasogeza sehemu
inayostahili,” alisema Mwalimu wa Taaluma.
Akitoa
nasaha kwa niaba ya wazazi wengine, Dkt. Wambuka Rangi ametoa rai kwa wanafunzi
kuendelea kuwa wachamungu ili kuepukana na matendo maovu ambayo yanapoteza
ndoto hasa za watoto wa kike.
“Tunaomba
muwe waadilifu na wasikivu kwa wazazi mtakapokuwa nyumbani, ilimuweze
kufanikiwa katika maisha yenu ya baadae”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.