Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amekutana na kufanya
mazungumzo na Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kupiga Vita UKIMWI,
TB na Malaria (GLOBAL FUND) Bwa. Andrew Hammond ofisini kwake Jijini Dodoma.
Dkt. Jingu amesema mazungumzo hayo yalilenga kujadili
masuala mbalimbali kuhusu sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora ya afya katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa serikali ya Tanzania itaendelea
kushirikana na mfuko huo kwani umekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha vifaa
tiba kama ilivyo azima ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais
Samia Suluhu Hassan ya kujenga miundo mbinu ya na
kuboresha masuala ya tiba kwa wananchi.
Naye Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa
kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND)
Bwa. Andrew Hammond ameishukuru Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko huo katika
kupiga vita maradhi ya Kifua Kikuu, Malaria na Ukimwi.
Ameahidi kuwa Mfuko wa Dunia utaendelea kuunga mkono
juhudi za Serikali za kukabiliana na magonjwa hayo hapa nchini kwa kuelekeza
rasilimali fedha kwa ajili ya kununua dawa pamoja na kuboresha mifumo ya utoaji
huduma ya afya.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.