Waziri
wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema
maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanatarajiwa kufanyika Mkoani Lindi katika Uwanja
wa Ilulu.
Mhe.
Simbachawene ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome, Jijini Dodoma.
Amesema
kuwa maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali kutoka
kwa wadau wa UKIMWI zikiwemo huduma ya
upimaji wa hiari wa virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine itakayotolewa kuanzia Novemba
24 hadi Desemba 01, 2022.
“Kauli
mbiu ya mwaka huu ni ‘Imarisha Usawa’
ambayo imetafsiriwa kutoka kauli mbiu ya kimataifa equalize, kaulimbiu hii
inahimiza kutilia mkazo uimarishaji wa usawa kutoa huduma za UKIMWI kwa makundi
yote ya wananchi na katika maeneo yote ya kijeografia kwa kuondoa vikwazo vinavyoondoa
usawa katika kufikia dira ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.”Amesema Mhe.
Simbachawene.
Pia
ameeleza kwamba maadhimisho hayo yatatumika kutathimini hali halisi na muelekeo wa
kudhibiti virusi vya UKIMWI, Kitaifa na Kimataifa pamoja na kuhamasisha viongozi
na jamii kuendelea kwa mapambano ya
kudhibiti virusi vya UKIMWI ili kujumuisha katika mipango yao ya maendeleo.
“Maadhimisho
haya yatatumika kama sehemu ya kuwaenzi wahanga wanaoishi na virusi vya UKIMWI
na kuwakumbuka wale waliopoteza maisha
kutokana na UKIMWI pamoja na kujali yatima ambao wametokana na vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo.
Vilevile Waziri Simbachawene ameiagiza Mikoa yote nchini kuandaa na kuadhimisha siku
hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine katika Mikoa na katika ngazi ya Wilaya.
“Maadhimisho
haya yatatumika kuhamasisha masuala mabalimbali muhimu ikiwemo utekelezaji wa azimio la umoja wa
mataifa la kutokomeza UKIMWI katika
kuhakikisha afua za kiafya zinapewa rasilimali za kutosha na mifumo ya kiafya
inaimarishwa”Amebainisha.
Aidha
amesema kuendelea kuwepo kwa siku hiyo muhimu kutasaidia upatikanaji wa dawa za kufubaza VVU, kuendeleza
utafiti wa kutafuta chanjo, kuimarisha afua za kinga dhidi ya maambukizi mapya
ya virusi vya UKIMWI na kuendelea kutekeleza afua za UKIMWI kwa kuzingatia na
kuheshimu haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.