Waziri wa Nchi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema ipo haja, mafunzo ya
itifaki na uratibu wa maadhimisho kufanyika kila mwaka.
Wito huo umetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene
wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa serikali yaliyohusu itifaki ya
viongozi wa kitaifa iliyowakutanisha Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika Mkoani Singida.
“Mafunzo haya yanapaswa
kuongezwa mada na kuongeza namba ya washiriki ili kujenga uelewa wa pamoja”
Ambao utasaidia kupata ufahamu
na ujuzi muhimu wa namna ya uandaaji wa Maadhimisho yanayohusu Idara na Taasisi
za Serikali kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa na kuzijua kanuni za kiitifaki ambazo
mtazitumia katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali kwenye taasisi zenu.
Awali Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amesema mafunzo yamelenga
kuwa na utaratibu ambao umekubaliwa, ambao unaleta matokeo chanya na watu wote
kuheshimu.
“Watendaji waliopokea mafunzo
sasa watasaidia katika maeneo yao; kitengo cha maadhimisho Ofisi ya Waziri
Mkuu, kwa sababu ndio Ofisi inayosimamia itifaki za viongozi”.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel
aliyekuwa mtoa maada wa huduma bora kwa mteja; ameshukuru serikali kwa
kuandaa mafunzo hayo ambayo yamesaidia kuwajenga watendaji kwenda kwa muelekeo
unaolengwa na nchi.
“Huu ni uwekezaji wa kifikira unaofaa, watendaji wakitoa huduma
bora kwa wananchi na kwa viongozi, mashauri yatapungua kwa sababu ya huduma
kuwa nzuri.”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.