Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amepongeza Tume ya kudhibiti
UKIMWI, Wizara ya Afya na Wizara ya TAMISEMI katika Mkakati wa kupambana na
Ukimwi kama janga la kitaifa.
Hayo yamesemwa Waziri na Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene Jijini Dar
es saalam, wakati wa uzinduzi wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani yenye Kauli
Mbiu inayosema Dangerous Inequalities iliyotolewa Mkurugenzi Mtendaji
anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS Bi, Winnie Byanyima.
“Serikali imedhamiria kuweka
usawa wa kijografia usawa kimazingira usawa kati ya watoto na wakubwa na usawa
wa kiuchumi ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma sawa ili wasiathirike na
wale walio athirika wapate huduma za matibabu lakini pia huduma sawasawa
kuhakikisha wanaendesha maisha yao.”
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi
Mtendaji anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS Bi, Winnie Byanyima amesema Tanzania
imejitahidi kupunguza Ongezeko la Maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kila
Mwaka kwa miaka kumi mfululizo.
“Tanzania Imejitahidi
kupunguza vifo vinavyosababishwa na UKIMWI na imekuwa ikifanya vizuri katika
mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI.”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.