Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema fedha zilizokuwa
zimetengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru
mwaka huu zitapelekwe Ofisi ya Rais – TAMISEMI nakutumika kujenga mabweni katika
shule nane za Msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini.
Taarifa hiyo na Waziri wa Nchi
Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika
mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Dodoma.
“Shilingi
Milioni 960,000,000/- (Tshs Milioni Mia Tisa Sitini) zitatumika kujenga shule ya msingi Buhangija
Shinyanga, Goweko Tabora, Darajani Singida, Mtanga Lindi, Songambele Lindi,
Msanzi Rukwa, Idofi Njombe, na Longido
Arusha.”
Ni dhamira ya dhati ya
Mheshimiwa Rais wetu ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki watu wenye
mahitaji maalum hapa nchini. Hili ni jambo kubwa la kishujaa na la kupongezwa
sana na Wananchi wote wa Tanzania.
Aidha Maadhimisho ya Sherehe
za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yatafanyika kwa Midahalo
na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa nchini
kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea
kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo
Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia. Hivyo hakutakuwa na Gwaride na shughuli
nyingine za Kitaifa.
Waziri
amesema, Maadhimisho ya MIAKA 61 YA UHURU yataadhimishwa kwa Kauli mbiu
inayosema “AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU”.
“Makongamano hayo yatatanguliwa
na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za
Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za
Wazee na makundi yenye mahitaji maalum”
Waziri ameelekeza Ofisi zote
za Serikali hapa nchini kupambwa kwa mapambo ya rangi za Bendera ya Taifa
pamoja na picha ya Mheshimiwa Rais.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.