Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema
nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa maendeleo ambayo ni shirikishi na
yamelenga watu.
Kauli hiyo imetolewa
na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara kilichofanyika Kibakwe Katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
“Katika ujenzi wa
maendeleo ukisema ujenzi wa sekondari za kata, ujenzi wa vituo vya afya ujenzi
wa barabara vyote vimetekelezwa kwa kushirikisha wananchi.”
Kauli mbiu ya miaka 61
ya uhuru ambayo inasema, Amani na Umoja ni nguvu ya maendeleo yetu.”
Imetusaidia kutimiza shabaha zetu.
“Mabadiliko ya kisiasa,
mabadiliko ya kiuchumi, Mhe. Rais amepeleka maendeleo hayo kwa watu na
maendeleo ya watu yanahitaji rasilimali fedha,” alisema waziri .
Sisi watanzania tuna
misingi yetu kila awamu inayoingia inategemea misingi ya awamu iliyopita
ndio maana tumefika hapa tulipofika.
“Watanzania
wanapenda furaha watanzania hawapendi hofu watanzania ni watii kwa mamlaka,
tuendelee kuheshimiana na kuipenda nchi yetu.”
Hata wenye mawazo
mbadala Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ndio maana
anazungumzia R-nne watu wawe na utaratibu wa maridhiano; maelewano, kujenga
upya, na kuendelea mbele.
“Tunaiona Tanzania
iliyobadilika sana kimaendeleo, lakini imebakia na misingi ile ile iliyoachwa
na waasisi wa Taifa letu katika mioyo ya watu.”
Tulivyopata uhuru
falsafa ya Baba wa Taifa alisema, Uhuru ni kazi ndio maana wananchi wamejikita
katika kufanya kazi.
Awali Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime amesema nchi imepiga hatua
kwenye miundo mbinu ya Mawasiliano.
“Ujenzi wa miundo
mbinu ya afya, ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, mabadiliko haya yameasisiwa na
viongozi wetu kutokana na Amani na utulivu uliojengwa na wazee wetu.”
Naye muwasilishaji
mada Mwl Charles Malugu amesema serikali ya awamu ya sita imefanya ujenzi wa
sekondari vyumba 20000, na ujenzi wa vyumba 3000 kwa shule shikizi ambao
utasaidia wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi wa darasa la kwanza
kuanza masomo bila kuwa na kikwazo cha aina yoyote.
“Serikali ya awamu ya
sita imeruhusu wanafunzi walikatisha masomo kutokana na ujauzito, kuendelea na
masomo ili wasikatize ndoto zao.”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.