Rais wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Watu wa Sahrawi, Mhe. Brahim Ghali leo amefanya ziara ndogo
katika mji wa Serikali Mtumba ambapo alitembelea jengo la Ofisi ya Rais
Menejiment na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Katika ziara hiyo ndogo Mhe. Rais Brahim Ghali
alikaribishwa na kuoneshwa Mji wa Serikali na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Uratibu Bwn. Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa
Serikali Bwn. Meshack Bandawe, ambapo walipata nafasi ya kuonyeshwa
kiwanja cha Ubalozi wa Taifa la watu wa Sahrawi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.