Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ametoa wito
kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini kuongeza nguvu
katika kutoa elimu kwa umma juu ya athari za dawa za kulevya kwa vijana na
wanachi wote kwa ujumla.
Hayo ameyasema
alipotembelea na kujionea eneo la Hekta saba ambalo linatarajiwa kujengwa jengo
la Makao Makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya
Kati, katika eneo la Itega Jijijni Dodoma.
“lazima tuvunje
ukimya na tuongeze udhibiti wa matumizi ya bangi, hatuwezi kudhibiti matumizi
ya bangi kwa kutegemea mamlaka pekee yake lazima tuweke mfumo na uratibu kwa
kuanza kudhibiti kuanzia ngazi ya kijiji, Kata na Wilaya.” Amesema
Simbachawene.
Tufike mahali
tuone tunauwa Taifa; Vitu vingi vinavyotokea kwenye familia, na matokeo ya
ajabu ya unyanyasaji msukumo wake ni matumizi ya madawa ya kulevya na ukipata
urahibu unashindwa kuisadia jamii, unashindwa kuwajibika kwenye familia
unashindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Waziri Simbachawene,
ameongeza kuwa aina mpya ya Urahibu wa kucheza Kamari (Kubeti) ambayo
inawakumba watu wote, na ina madhara kama urahibu wa madawa ya kulevya, lazima
tujipange.
Kila mmoja ni shahidi
watu wanapokuwa wanafanya Kamari ya kubahatisha, kwenye michezo ya mpira, hata
kufanya kazi hawawezi, muda wote ni kuangalia mkeka tuu(kubeti)
Aidha kuna umuhimu wa
kuziunganisha kwa kuziimarisha Taasisi zetu hizi za Hospitali ya Taifa ya Afya
ya Akili Mirembe na Mamlaka wa Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kisera
na kisheria ili ziweze kushirikiana vizuri katika utendaji wa kazi.
Naye Kamishna wa
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Jenerali Gerald
Kusaya amesema katika Mwaka huu wa fedha serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu imeweza kupeleka Vyuo vya Ufundi warahibu walioachana na matumizi ya
dawa za kulevya wapatao 245 wanaolipiwa ada zote na Ofisi ya Waziri Mkuu na
kila mmoja amechagua kitu anachotaka kusoma ili watakapomaliza warudi mtaani na
waweze kuanza kujitegemea na kujenga uchumi wa nchi.
Katika kuhitimisha
ziara hiyo kamishna Jenerali Kusaya ameomba serikali kuwasaidia warahibu
wanaohitimu mafunzo ya Ufundi stadi na stadi za kazi kupewa vitendea kazi
vitakavyowasaidia pindi watakaporudi kwenye jamii yao
Jumla ya warahibu
wapatao 12,800 wanatarajia kuhitimu mafunzo kutoka kwenye vyuo vya ufundi wakiwa
na ujuzi wa stadi mbalimbali za kazi na kuweza kujitegemea na kujenga uchumi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.