Serikali Kupitia Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu imetoa msaada kwa wananchi walioathirika na
Maafa ya Mafuriko ya Maji Mkoani Mbeya, yaliyosabisha nyumba kubomoka,
kuharibika kwa vifaa, vyakula, uharibifu wa mifugo na mazao yaliyoko
mashambani.
“Msaada huo unajumuisha Magodoro
300 kwa kuanzia, mablanketi 1200 ya wakubwa na wadogo, mikeka 600, madumu ya
maji, sufuria bakuli sahani pamoja na vijiko kwa kila familia ambayo imeathirika.”
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene
alipotembelea maeneo yaliyoathirika wa mafuriko ya mvua katika kata saba Mkoani
Mbeya kutokana na Mvua zilizonyesha
terehe 07/01/2023.
“Kwa mujibu wa sheria no. 6 ya
Maafa ya Mwaka 2022 sisi kama Ofisi ya Waziri Mkuu tunayo dhamana ya
kuwaunganisha wadau ili kuwasaidia watu walioathirika na tutafanya hivyo kwa
kutumia Ofisi zetu za Mkoa na wilaya, naomba wadau wote wa ndani na nje ya Mkoa
wa Mbeya kutusaidia ili kuhakikisha watu hawa wanarudi katika hali yao.”
Natoa pole kwa wote
walioathirika, TARURA kwa kushirikiana TANROAD Halmashauri ya jiji la Mbeya na Halmashauri ya Mbeya vijijini
wahakikishe wanaenda kuona kwenye vyanzo kuangalia ni eneo gani maji yametoka
kwenye mkondo wake wa asili.
Akimkaribisha Waziri wa Nchi, Mbunge
wa jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Tulia Ackson ameishukuru serikali kwa mchango iliyoutoa kwa waathirika wa mafuriko ya Mvua Mkoani Mbeya .
“Naomba sisi kama Halmashauri
tusitoe vibali vya ujenzi kwenye maeneo
ambayo ni mikondo ya maji, kwa sababu athari za mafuriko zinarudisha nyuma maendeleo ya uchumi kwa wananchi”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.
Juma Homera katika taarifa yake amesema watu waliopata athari za mafuriko ya
maji, kaya 281 zenye watu idadi ya watu 1405 ambao wanahitaji chakula takribani
tani 50 kwa miezi mitatu ili ziweze kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.