Serikali kupitia Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) imetoa misaada ya kibinadamu kwa kaya 184 za
kata ya Kitaya Halmashauri ya wilaya ya Nanyamba na kaya 160 kwa kata ya
Michenjele Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.
Zoezi hilo limeongozwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe, Jenista
Mhagama Mkoani Mtwara, amesema kwa kutumia sheria no 6 iliyotungwa mwaka 2022
ya usimamizi wa maafa, kazi yetu ni kufanya tathimini na kutoa Mkono wa pole
kwenye Majanga yanayohusu binadamu mahali popote.
“Nitoe wito kila yanapotokea
majanga na maafa, kwanza liwe jukumu letu kufarijiana kwa karibu; na kutoa
taarifa za dalili za majanga yanapotokea, na kuangalia ni mambo gani ya msingi
yafanyike ili kurudisha hali katika utaratibu wa kawaida” alihimiza.
Waziri Mhagama amesema, tumepokea
tathimini iliyowakilishwa ikionesha madhara yaliyojitokeza kwa wananchi katika
eneo hili katika maeneo kadha kwa kadha katika makazi, chakula,na nyenzo za kufanyia shughuli za kiuchumi
Amefafanua kwamba Serikali
imekuja kutoa Mkono ili tuweze kushirikiana na nyie katika kujibadilishia hali
katika kipindi hiki chote, “nikweli Serikali imeendelea kuwa na nyie kwa nguvu
kubwa na ya ziada zaidi,” alisema Mhe. Waziri
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassani kwa kutushika Mkono wananchi
yanapotokea majanga ya kibindamu, yanapotokea mafuriko, na vinapotokea vimbunga,
tunajisikia faraja.
Tumepokea magodoro 190 tumepokea
ndoo kubwa 380, na ndoo kubwa za lita ishirini 190, tumepokea blanketi za watoto
190 na blanketi za watu wazima 380 na mikeka 380 na mabati 5700 na kaya
zinazostahiki ni 184 zilizoordheshwa kwa sasa katika Halmashauri ya wilaya ya Nanyamba.
Kanali Ahmedi ameongeza kusema
Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Ilipokea vifaa vya msaada wa kibinadamu kwa
waathirika 160, tuna mabati 4800 kuna magodoro 160, mikeka 320 na mablanketi
320, ndoo kubwa za lita ishirini 320 na tayari zimeundwa kamati mbalimbali kwa
ajili ya kuhakiki
Naye Mbunge wa Nanyamba Mhe.
Abdallah Chikota amesema Tunashukuru kwa msaada wa kibinadamu na kipekee
nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu
Hassan kwa sababu asiyeshukuru kwa moja hata kumi hawezi kushukuru.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.