Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama,
amekabidhiwa kipande cha sehemu ya ujenzi wa uwanja wa mashujaa, katika Mji wa
Serikali Mtumba, Jijini Dodoma mapema Julai 2, 2023.
Ujenzi huo unaotekelezwa na
kampuni ya SUMA JKT,Umekamilisha kipande cha
sehemu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja wa Gwaride ambao unategemewa
kutumika katika Maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Akiwa kiwanjani hapo Waziri
Mhagama alisema, Serikali pamoja na kuhamia Dodoma imejenga miundombinu yenye
hadhi ya makao Mkuu ya Serikali, na jamii inashuhudia majengo ya Serikali
makubwa na miondombinu mingine ikiendelea kukamilishwa.
Akiongelea Ujenzi wa Uwanja
huo, Waziri Mhagama alisema, ujenzi utakapo kamilika utakuwa ni wa mfano Barani
Afrika.
"Eneo hili ni sehemu ya
kwanza ya ujenzi wa eneo la maadhimisho ya uwanja wa mashujaa, (Parade Ground)
ambayo itakuwa na Mnara wa Mashujaa, wenye ubora na viwango vya juu kabisa.”
Alieleza Mhe. Mhagama
Aliendelea kusema kuwa, awamu
ya pili itakuwa na bustani kubwa, ambayo itakuwa na mvuto wa aina yake, na
tayari Taasisi mbali mbali za Serikali zimeonesha nia ya kuwekeza na
kushirikiana, kuhakikisha kutakuwa na bustani hiyo yenye migahawa, viwanja vya
michezo na burudani mbalimbali, ambazo zitakuwa katika eneo hilo ambao leo
amekabidhiwa kipande kidogo tuu kama sehemu ya kwanza ya ujenzi.
Alifafanua zaidi kuwa, sehemu
ya tatu itahusisha ujenzi wa mnara mrefu wa zaidi mita 110 ambao utakuwa mnara
wa kwanza Barani Afrika, ambao utakuwa ni kivutio kwa watalii na kuongeza pato
la Taifa.
Kwa Upande Katibu Mkuu wa
Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi alisema uwanja huo utakapokamilika utaongeza uzuri
na ubora wa Jiji la Dodoma na Serikali itahakikisha kwamba mnara pamoja na
uwanja wake unakuwa wa kupendeza na kuwa na mvuto wa kipekee huku akizishuruku
sekta nyingine zilizoonesha ushirikiano katika utekelezaji wa ujenzi huo na
kuhakikisha miundombinu muhimu inapatikana kwa wakati.
Awali akizungumza katika
makabidhiano hayo, Katibu wa Kikosi kazi cha Taifa cha kuratibu Serikali
kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe, alisema ujenzi huo umezingatia suala la
mpango kabambe wa ujenzi wa Mji wa Serikali na kazi ya ubunifu wa awali
ilifanywa kwa kina na wataalam kutoka chuo kikuu cha Ardhi, TPA, NHC na SUMA JKT.
Naye Mwakilishi wa kampuni ya Ujenzi kutoka SUMA JKT kanda
ya Kati Meja Samweli Jambo, alisema ujenzi huo umefuata taratibu zote za
upimaji na viwango.
“Tulifanya kazi
usiku na mchana kuhakikicha tunatekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri ya kukabidhi
kipande hiki kwa wakati.” Alieleza Samweli
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.