Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na (Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Muhagama amesema maonesho ya kilimo ya Nane Nane ni njia pekee ya wakulima kuweza kujifunza mbinu bora za kilimo cha kisasa na matumizi ya zana bora za kilimo zinazoweza kuleta mafanikio katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara nchini.
Aliyasema hayo mapema , alilpokuwa katika Shehia ya Dole Kizimbani alipokuwa akifunga
Maonesho ya wakulima Nane Nane yaliyo washirikisha wadau kutoka sekta binafsi
na wakulima 275 wajasiriamali, taasisi binafsi na za Serikali.
“Serikali ya Mapinduzi ya
Zanziba chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Hussen Ali Mwinyi inafanya juhudi kubwa katika kuibadilisha nchi ili
kuweza kuleta madiliko katika sekta za uzalishaji wa chakula na kuweza kukidhi
mahitaji ya wananchi wake” alibainisha.
Zanzibar imepiga hatua nzuri
na matokeo ya Maonesho yatawezesha wakulima kujifunza vitu vipya na kwenda
kuleta mapinduzi ya kilimo ambapo wakulima wataźalisha kwa wingi mazao ya
biashara ambayo yataongeza mnyororo wa thamani wa mazao na kuweza kufanya
baishara katika soko la ndani na nje ya nchi.
Akiongea katika maonesho hayo,
katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo amesema
Maonesho hayo yenye lengo la kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima yamedumu
kwa siku 10 na kugharimu kiasi cha Shilingi
Milioni Mia Tano fedha za kitanzania.
Kwa upande wake Waziri wa
Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis ameishukru
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano kwa mashirikiano yao
na kuyawezesha maonesho ya kilimo kwa mwaka 2023 kufanikiwa
Aidha aliwashukuru wadau na
wananchi wote waliochangia na kuwaomba wakulima kuzidisha bidii na kuja na
mbinu mpya za kilimo katika maonesho yajayo
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.