Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulika na (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, Ameitaka
Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali,
kuharakisha kutengeneza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Utendaji wa
Shughuli za Serikali Pamoja na kukamilisha na kuzindua haraka Mwongozo wa
Ufuatiliaji na Tathmini ndani ya nchi utakaotumika na Seriali kwa ujumla,
Wizara, Taasisi na maeneo yote ya Utendaji kazi ndani ya Serikali.
Ameyasema hayo Jijini Arusha, alipofungua
Mkutano wa Mazingativu uliyohusisha, Viongozi, watumishi wa Ofisi hiyo Pamoja
na Taasisi zake.
Sambamba na hilo, Pamoja na
kuonesha Imani wa Mkurugenzi wa Idara hiyo mpya, Waziri Mhagama aliitaka pia
idara hiyo kuwa na Ubunifu “Jaribuni kununua mifumo, miundo na taratibu za
kufanya ufuatiliaji na Tathmini kutoka kwenye mataifa mengine, ili tuweze
kuitangaza Taifa letu kwa kazi hili kuwa tunaweza kufanya vizuri” Alisisitiza
Waziri Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama alisema
anahitaji kupata taarifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Ofisi yake
na Serikali kwa ujumla wa kila robo mwaka ikiwa ni katika kuboresha Eneo hilo.
Akizungumzia kuhusu
Uchapishaji wa Nyaraka za Serikali, Waziri Mhagama alisema katika eneo hilo,
katika mwaka huu Mpya wa Fedha 2023/2034, Serikali imejiwekea mkakati wa
kuongeza Maduhuli na mapato ya yake kupitia Mpigachapa Mkuu wa Serikali, ambapo
ujenzi wa Mradi wa Mkakati wa kiwanda kipya cha Mpigachapa Mkuu wa Serikali
Umefikia asilimia 97% na “Tumeshaanza kufanya manunuzi ya mashine za kisasa, na
tumeshafufua mashine ambazo zilikuwa zimehariba.
Nisisitize Chapa muendeshe
kiwanda kwa Ubunifu, jengeni fikra mpya boresheni mifumo miundo na namna ya
uhifadhi na uchapaji wa nyaraka za Serikali, nataraji kiwanda hiki kinaweza
kikajiuza na kinaweza kikapata soko la nchi za kusini mwa Afrika SADC na katika
na Soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,
pale mnalo jambo na kazi kubwa ya kufanya, na mazingativu haya yawasaidie
kujiongoza na kupata picha na fikra ambazo zitatuvusha.” Alisisitiza Waziri
Mhagama
Akiongea katika Mkutano huo wa
Mazingativu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt Jim
Yonazi alisema kuwepo kwa Ofisi hiyo Jijini Arusha katika Mkutano huo ni kutokana na nia ya Ofisi hiyo kuhakikisha
kwamba inatenda majukumu yake kwa umakini na kwa utimilifu ikiwa ni pamoja na
Uratibu wa shughuli za Serikali kwa ujumla na kwenye maeneo mengine.
“Tunaweza kujifunza kutoka
hapa ndani ya nchi mambo mengi na tukatumia ubunifu na wataalam wa ndani katika
utendaji na hakuna mtu anaweza kuwa mbunifu katika mazingira yenye stress,
hivyo tunaweza kuweka mazingira wezeshi kwa watumishi na kukuza na kuongeza
uelewa katika utendaji.”Alisema
Kwa kutekeleza Agizo la Mhe. Waziri Mhagama,
Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini wa Ofisi Hiyo Bi. Sakina
Mwinyimkuu alisema, kikosi kazi kitakaa haraka ili kuweza kuandaa mwongozo wa
ufuatiliaji na Tathmini na kuhusiana na
kuwa na Mfumo wa Ufuatiiaji na Tathmini, Mkurugenzi alisema kazi hii inafanyika
kwa kushirikiana na Taasisi ya Serikali Mtandao (Ega) na maandalizi ya kujengwa
kwa mfumo huo yanatarajiwa kuanza.
Kwa Upande wake Mpigachapa Mkuu wa Serikali
Bw. George Lugome alisema, kama Idara imejipanga hasa kwa watumishi kuhakikisha
wanafanya kazi katika ubora wa hali ya juu na kuhakikisha, watumishi watapata
mafunzo ya kuendesha mashine mpya za kisasa, kuongeza idadi ya watumishi wenye
sifa na ueledi katika endeo hilo la uchapaji “Ili kuweza kuendana na mabadiliko
ya teknolojia, ni lazima pia tuchape nyaraka za Serikali kwa kufuata Ubora na
kuweka alama za usalama kulingana na teknolojia zilizopo,na tumeshaanza
mikakati ya namna gani ya kushirikiana wenzetu wenye utaalam wa masuala ya
usalama katika nyaraka mbalimbali.” Alifafanua
Mada mbalimbali zinawalishwa katika Mkutano huu wa
mazingativu ni Matarajio ya washiriki
wengi kuwa, mkutano huo utawasaidia, kuboresha utendaji wa kazi, kujifunza,
kupata ubunifu katika maeneo yao ya
kazi, kuongeza bidii zaidi na hali ya utendaji katika kazi unaoendana na
sayansi na teknolojia.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.