Naibu Waziri Mkuu na
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kama Serikali haitafanya
Tathmini ya Shughuli zake haitakuwa na uwezo wa kujipima na vihatarishi vya
utekelezaji wa mipango yake.
Mhe. Naibu Waziri Mkuu
Dkt. BITEKO ameyasema hayo mapema leo jijini Arusha alipofungua Kongamano la
Pili la Kitaifa la Ufuatilijai, Tathmini na Mafunzo ambapo amesema Serikali
imegawanyika katika maeneo mengi kama vile Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
hivyo ufuatiliaji na tathmini ni eneo muhimu na linalopaswa kutiliwa mkazo.
Kutokana na umuhimu huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan anasisistiza Serikali kuwa na Uratibu wa shughuli zake.
“Unaweza kukuta Serikali za Mitaa na Serikali
kuu kila mtu anafanya jambo lake hakuna vinavyosomana, tujifanyie tathmini ili
tusije kuwa watu wa kuduwaa kunini hili limetokeaje.” Alisisitiza
Dkt.Biteko aliongeza
kusema kuwa asiyejifanyia tathmini atakuwa ni mtu wa hasara hivyo kujifanyia
tathmini kunaifanya serikali kubaini matatizo mapema na kuweza kuyatafutia
ufumbuzi kabla hayajaleta hasara. Dkt. Biteko ametoa wito kwa washiiriki wa
kongamano hilo hasa watendaji wa serikali kufanya ufuatiliaji na tathmini bila
kuweka mbele rasilimali fedha.
Sambamba na hilo,
Naibu Waziri Mkuu Dkt. BITEKO amewataka maafisa masuhuli wote nchini
kuviwezesha vitengo vya ufuatiliaji na tathmini katika wizara na taasisi zao
kwa kuhakikisha kunakuwa na wataalamu wa kutosha, vitendea kazi na rasilimali
fedha ili viweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande wake Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulika na masuala ya (Sera, Bunge na
Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema, wakati kongamano hili likifanyika kwa
mara ya Pili hapa nchini, Serikali imefanyia kazi kwa Asilimia mia, (100%)
utekelezwaji wa agizo la uanzishwaji wa Idara za Ufuatilijaia na Tathmini
katika Wizara na Serikali.
Awali akiongea wakati
wa Ufunguzi wa Kongamano hilo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) Dkt. Jim Yonazi, alisema kwa kufuatilia mwendeno wa utekelezaji wa
kujipima matokeo, Taasisi za Umma zinaweza kujihakikishia kuwa zipo katika njia
sahihi za utekelezaji katika kufikia malengo yake, hivyo Ufuatiliaji na
Tathmini ni njia nzuri ya kujifunza na kuwajibika.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.