Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga
ameupongeza uongozi wa Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa mbegu za
kilimo (ASA) kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuzalisha na uendelezaji wa mbegu
nchini huku akiwasihi kuendelea kuzingatia ubora na weledi katika majukumu ya
kuzalisha mbegu bora hizo ili kuendelea kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha
nchini.
Ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya
kikazi kufuatili shughuli za utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya
Kilimo na Uvuvi ya AFDP ambayo inaratibiwa na ofisi yake na kutekeleza katika
mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Morogoro.
Akiwa katika ziara hiyo alitembelea Kituo cha
Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira, Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na
Uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) Pamoja na Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu
Tanzania (TOSCI) zilizopo Mkoani
Morogoro.
Mhe.Ummy amesema upo umuhimu wa kuendelea
kuunga mkono Programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi nchini kwa
kuzingatia inaongeza tija hasa katika kuhakikisha kunakuwa na mbegu bora
nchini.
“Ofisi ya Waziri Mkuu tunaendelea kufanya
uratibu na kutathmini ya programu hii ambayo ni ya miaka sita hivyo endeleeni
kufanya kazi vizuri, kwa weledi huku mkiunga jitihada za Mhe Rais za kuona
Tanzania inakuwa ghala kubwa la chakula, Serikali haita waacha nyumba,
inaendelea kuunga mkono jitihada hizi.” alisema Mhe. Nderiananga
Aidha aliwataka kuendelea kuzingatia ubora na
viwango katika utekelezaji wa majukumu ya uzalishaji wa mbegu bora na
zinazoendana na mahitaji halisi.
“Eneo la mbegu ni muhimu sana, bila kuwa
na mbegu nzuri hatuwezi kuwa na matokeo ya chakula kizuri, hivyo ninawapongeza
mnafanya kazi nzuri endeleeni maana tunategemea sana sekta yetu ya kilimo ili
kuendelea kuwa na uhakika wa chakula nchini,”alisisitiza.
Kwa upande wake Mchumi Mwandamizi kutoka wa
Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mbegu za Kilimo (ASA) Bw.
Edmund Kayombo akizungumza kuhusu wakala hiyo amesema umeendelea kutoka huduma
za kuongeza uzalishjaji na usambazanji mbegu bora, kuhamasisha sekta binafsi
kushiriki katika uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora, kuhamasisha wakulima
kutumia mbegu bora na kushirikiana na kituo cha utafiti ili kuhakikisha mbegu
mpya zinazaliwashwa na kusambazwa kwa wakulima.
“Wakala wa Mbegu za kilimo una jumla ya
mashamba 14 ikiwemo mashamba ya kilimi yaliyopo Nzenga, Msungula (Kasulu),
Chalinze, Nane nane - Morogoro, Tanganyika, Dabaga kilosa, Arusha (Tengelu),
Namtumbo (Songera), Njombe, ambayo yanajumla ya ukubwa wa hekta 16,909,”
alisema Kayombo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.