Katibu Mkuu Kiongozi Mhe.
Balozi Dkt. Moses Kusiluka ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Uratibu na
Usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Ametoa pongezi hizo mapema
leo, alipokuwa katika ziara maalum ya Makatibu Wakuu ya kutembelea mji wa
Serikali Mtumba Dodoma ambapo alisema mafanikio ya mradi huu wa ujenzi wa Mji
wa Serikali ni kukamilika kwa ukamilifu wake akitolea mfano ujenzi wa Uwanja wa
Mashujaa kuwa ni alama kubwa ambao utatumika kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na
wageni kujifunza nini ambacho Tanzania imefanya.
“Tunathamini kazi yenu kubwa
sana mnayofanya, kama tulivyosema awali kwenye Wasilisho, hii kazi inahitaji
Uratibu kwa Sababu ni kazi ya Serikali, siyo kazi ya mmoja kuwa amemaliza na
wengine kujisikia vibaya, tunashukuru kwa kutupitisha kwenye kazi kuanzia
mwanzo, tumeona juhudi kubwa za wataalamu wetu na wasimamizi lakini pia tumeona
kazi kubwa iliyopo mbele na tunatambua kwamba baadhi ya wadau wanakaribia
kumaliza kazi zao.” Alisema Mhe. Balozi Kusiluka.
Aliendelea kusema kuwa bado kuna muda wa
kutosha wa kutatua Changamoto ndogo zilizobainika katika ziara hiyo; na
kusisitiza kuutazama mradi huo kwa ujumla wake kama Serikali moja, na kazi ya
uratibu ikiendelea lakini pamoja na kuimarisha timu ya wataalamu wa ngazi zote
katika ujenzi na kuwasikiliza, “Ni Fursa Pekee ambayo tumepewa ya kujenga Makao
Makuu ya Serikali mapya na Serikali
imetoa fedha nyingi kwa hivyo ni lazima sisi wataalam tufanye kazi
inavyopaswa.” Alisisitiza.
Alimshukuru Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za
kutekeleza mradi huo, na kuwapa uhuru wataalam kufanya kazi ya kitaalam
inavyopaswa, na kushauri wadau wengi kushiriki katika kazi hiyo pamoja na
kujadili mambo ya kitaalam ili watu wengi waweze kujifunza
Kwa Upande wake Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz alisema swala la
ushirikishwaji wa wataalam katika ujenzi wa mji wa Serikali ni swala la muhimu
sana, na wadau mbalimbali wanashirikishwa kwa ajili ya kuja kuwekeza katika
maeneo mbali mbali ambayo yametengwa
katika mji huo wa Serikali,na majengo hayo ya Mji wa Serikali yapo katika hatua
mbalimbali za ukamilishwaji.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.