Viongozi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wamekagua maandalizi ya kuelekea Kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Desemba 1, 2023 katika Viwanja vya
Morogoro Sekondari ambapo maandalizi hayo yamekamili. Katika ukaguzi huo
waliongozwa na Mhe. Jenista Mhagama ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ya
uratibu.
Ikumbukwe maadhimisho ya siku
ya UKIMWI Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema
“Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI”.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.