Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea
kujitokeza kupima VVU kwa hiari ili kujua hali zao ili kuendelea kuishi kwa
kuzingatia matokeo, kwa wale ambao hawatakutwa na maambukizi ni nafasi kwao
kuendelea kuishi ili wasiambukizwe na wale ambao watakutwa na maambukizi wana nafasi kuendelea kuishi kwa kutumia dawa
za kufubaza.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa
kikao cha pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,anayeshughulika na Sera,
Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Kighoma
Malima kuhusu kuelekea maandalizi ya siku ya UKIMWI kitaifa, katika kikao
kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Ameongeza kusema tafiti zote
za miaka mitano zimeonesha wanaume hawajitokezi kupima, na hawajitokezi kuanza
kupata dawa, na hivyo kusumbuliwa sana na magonjwa Nyemelezi yanayotokana na
virusi vya UKIMWI.
“Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
upo ni wajibu wa kila Mwananchi kuendelea kuchukua tahadhari,” alibainisha
Aidha kauli mbiu yetu inyosema;
JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI inatuhamasisha jamii yenyewe
ndio iongoze mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI
Akizungumzia kuhusu malezi,
ametoa rai kwa wazazi kukaa na familia na kuwaelimisha uwepo wa tatizo hili la
UKIMWI.
“Tunajukumu kubwa la kuendelea
kutoa malezi bora kwa watoto wetu na kuwajengea misingi ya tabia njema”
alifafanua
Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Mhe. Adam Kighoma Malima amesema maandalizi kuelekea wiki Maadhimisho ya siku
ya UKIMWI yanaendelea vizuri
“Lengo ni kupeleka ujumbe kwa
wananchi, huku tukitupia jicho kwa kundi la vijana na kwa kushiriki kwao
itasaidia kupeleka ujumbe kwa vijana wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki,”
alisema
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.