Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeahidi kutoa kiasi cha shilingi Millioni 20 ili kuimarisha kivuko cha kivuko cha Magole/Mwanagati kilichopo katika kata ya Mzinga Halmashauri ya Ilala Mkoani Dar es salaam ili kiweze kupitika muda wote.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe, Jenista Mhagama
wakati akizungumza na wakazi waliojitokeza katika eneo hilo la kivuko
liloathirika na Mvua wakati wa ziara yake iliyolenga kupata taarifa
zilizochukuliwa na Kamati ya Mkoa ya Maafa juu ya kudhibiti madhara ya zaidi mvua
yanayoweza kujitokeza.
Ameongeza kusema kazi ya kuimarisha
kivuko ifanywe na wakala wa barabara vijijini TARURA haraka iwezekanavyo.
“Kivuko hiki kitakapokuwa
kinapitika muda wote hakitarudisha juhudi ya kwenda na Mpango wa pili wa muda
mrefu wa kujenga daraja la kudumu,”alibainisha
Waziri mhagama alisema kuwa
serikali inatamani kuona shughuli za wananchi zifanyika bila kusimama;
tunatamani watoto wetu waende shule, tunatamani kina mama wajawazito waende
kupata huduma za afya kwa wakati, tunapenda wananchi wajisikie serikali yao
inawajali, alisema Waziri.
“Tunataka tutengeneze daraja
livutie machoni pa watu, kile matumaini kwa watu kwamba hii ni nyota ya Mhe.
Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan na wananchi washirikishwe kiasi cha kutosha,”
alifafanua
Waziri Mhagama alielekezaTARURA
kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa
na kwa hofu ya mungu, kwa sababu mnasimamia uhai na maisha ya watu na sisi
tunawaamini na tunawategemea.
Katika hatua nyingine Waziri
ameomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko; hali
ya mvua inaweza kutupelekea kwenye magonjwa ya kuhara, magonjwa ya malaria.
Aliwaasa wananchi kuendelea
kusafisa vichaka na kujenga utaratibu mzuri wa kusafisha mazingira yetu na kila
mmoja awe askari wa mwenzake na kuhakikisha mifereji yetu inakuwa safi na
mapito ya maji yanakuwa wazi.
Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Mhe. Albert Chalamila alisema Mkoa wa Dar es salaam umeathiriwa
na wa ujenzi wa kutawanyika, hivyo kasi ya ujenzi wa miundombinu imekuwa
gharama kubwa, lakini lazima hilo lifanyike kwa sababu ni huduma kwa
watanzania.
Wataalamu wetu wamekuwa wakisanifu
ramani za daraja lakini bado hatujapata fungu la fedha kwa ajili ya ujenzi wa
daraja, na hapa tunahitaji mkakakati mkubwa wa kuzuia mto kutokula kingo zake.
:Tunajitahidi kuhakikisha
wananchi hawajengi mabondeni; na kulinda mito dhidi ya shughuli za kibinadamu, ikiwa
ni sambamba na kuhakikisha tunaunganisha
miundo mbinu ya mawasiliano ili mambo yaweze kwenda vizuri,” alifafanua Mkuu wa
Mkoa.
Naye diwani wa kata ya mzinga
Mhe Jackob Izack amesema kero ni kubwa na kumshukuru sana waziri kwa kuja,
mipango ilikwisha pangwa, mahitaji ya wananchi ni mikubwa na kuna wananchi zaidi
ya elfu ishirini wanapita kila siku.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.