Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa watumishi
walio chini yake kufanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana bila kutengeneza
makundi.
Ametoa rai hiyo Mkoani
Morogoro wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge na uratibu kilicholenga kujadili Taarifa ya Bajeti ya
2023-2024 ya Ofisi hiyo.
Waziri Mhagama alisema, Kuna
kila sababu ya kufanya maamuzi ya pamoja ya ushirikishwaji ili kuweza kupata
mafanikio kwenye idara na vitengo, kama viongozi wenu wanavyofanya kazi vizuri
kwa kushirikiana.
Aliendelea kusema kuwa hata
kama inafikia wakati Mtendaji hayupo kwenye Idara au kitengo kuwe kuna Mtu
anayeweza kufanya kazi kwa viwango na uwezo huo huo ili mambo yaweze kwenda
vizuri.
“Tukifanya kazi kwa umoja na
ushirikiano tukifanikiwa tuwe tumefanikiwa wote na tukianguka tujue tumeanguka
wote na tujipange ili kujua sababu ya kuanguka na tuweze kujipanga."
Alibainisha.
Aidha, Waziri Mhagama alisema
anafarijika na utendaji wa kitaasisi na kuwaomba watumishi kuendelea kuimarisha
utendaji wa kitaasisi ambao unatoa fursa kwa kila mtu kuwa ni sehemu ya
mafanikio na ufanisi wa taasisi.
“Wale ambao Mnamadaraka kwenye
Idara Vitengo au Taasisi zetu Muhakikishe Mnajenga moyo wa kukuza watumishi
walio chini yenu, kwa kuwapa fursa ya kukua kielimu ndani ya ofisi, kukua kiujuzi
na kukua kiubobezi." Alihimiza.
Alibainisha kuwa Watumishi wa
umma ni rasilimali muhimu, ya kuendesha rasilimali nyingine na kusema kuwa ni
lazima tuiratibu vizuri Rasilimali hiyi na kuilinda kwa nguvu zote ili kuweza
kupata mafanikio tuliyoyakusudia.
Waziri alisema; Rais wa awamu
ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa aliwahi kusema,” jambo muhimu kwa mfanyakazi si
muda anaotumia kufanya kazi,bali kiasi cha kazi anachoweza kufanya katika muda
aliopewa."
Alisema Kuna kila sababu ya
kuanzaa kujipima wenyewe hasa katika kuelekea kuanza mwaka 2024, ili kujua
kiasi cha kazi tuliyoifanya na ufanisi wake kila siku anayoshiriki kama
mtumishi wa umma katika ofisi ya waziri Mkuu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, amesema vikao vya
wafanyakazi ni tamko la kisheria ambalo chimbuko lake ni Hayati Baba wa Taifa
mwalimu Julius Nyerere, Rais wa awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alilolitoa katika tamko no 1 la mwaka 1970 linalohimiza ushirikishwaji
kupitia Baraza la wafanyakazi.
"Baraza ni kiungo muhimu
kati ya wafanyakazi na Menejimenti na Ofisi ya Waziri Mkuu, tutaendele kuwa
vikao hivi vya baraza la wafanyakazi kwa mujibu ya miongozo.
Awali akitoa salamu Katibu wa
TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Samwel Nyungwa ameipongeza Menejimenti ya Ofisi ya
Maziri Mkuu, kwa kutekele za Sera ya ushrikishwaji kikamilifu,
Chama cha wafanyakazi
kinaamini hakuna haki bila wajibu, tunaangalia namna tunavyopata haki na namna
ambavyo tunatekeleza wajibu katika kuhakikisha mipango iliyopangwa inakamilika
sawasawa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.