Padre Emmanuel Mtambo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska amesema Kanisa linawajibu wa kuchangia watanzania wenzetu waliopata janga la mafuriko ya Mawe na Matope kutoka Mlima Hanang’.
Alisema Parokia ya Mwenyeheri
Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja cha Ndege kupitia kamati ya Caritas ambayo
inashughulikia wanaohitaji, leo jijini
Dodoma imetoa hundi ya shilingi milioni 5 ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na serikali
kusaidia waathirika.
“Kama Parokia na Kanisa; tunapaswa
kufanya sehemu yetu, kupitia michango yetu tunayotoa katika akaunti ya Caritas”
alifafanua
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.