Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama
ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuzilinda tunu za umoja wa kitaifa za
utulivu, amani na ushirikiano.
Rai hiyo ametoa wakati
akimwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Samia Suluhu Hassan Katika Misa ya kuweka wakfu Askofu wa Jimbo la Njombe Dkt.
Eusebius Samwel Kyando iliyofanyika Mkoani Njombe
Waziri amesema kuwa tunu hizo
ndizo zinazotambulisha Taifa letu la Tanzania duniani na ulimwenguni
kote.
"Tunu hizi zilindwe kwa
kuzingatia umuhimu wake, pia Serikali inashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea
kuliombea Taifa, tunaomba muendelee kuliombea bila kuchoka "
alifafanua Waziri
Aidha viongozi wa dini
mmekua mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa katika hali ya
utulivu mstahimilivu na Mhe. Rais amekuwa mstari wa mbele Kati Jambo hilo.
"Niwaombe Sana Viongozi
wa dini tuendelee kukemea pale tunapoona kuna viashiria vya watu wachache
kuvunja amani, utulivu umoja na mshikamano wa Nchi yetu," alihimiza
Aidha aliitaka jamii kuungana
na Serikali katika kupaza sauti juu ya matendo maovu na hasa mauaji na ukatili
wa kijinsia, imani potovu ambazo zinapelekea mauaji na unyanyasaji wa watoto.
Aliongezea kuwa Falsafa ya
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ya 4R, inalenga sekta zote na
utendaji wote ndani ya serikali, na utendaji wa waumini na taasisi zake za
kidini hivyo, aliwaombe viongozi wa dini kuunga mkono falsafa hiyo hasa katika
ustahimilivu na maridhiano.
"Dhamira ya Mhe. Rais
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ni njema na inahitaji kutiwa moyo ili iweze
kusonga mbele hasa kwa vitendo," alisisitiza
Akizungumza kuhusu masuala ya
uchaguzi na fursa zilizopo aliisihi jamii kuwa tayari kuitumia kwa
kushiriki vyema uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.
“Uchaguzi wa serikali za mitaa
kwa mwaka huu 2024, niwaombe wananchi tuweze kushiriki zoezi la uchaguzi huo
kwa amani na utulivu,” aliongeza
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka ameomba viongozi wa dini kwa kushirikiana
na serikali kwa pamoja kuunga mkono jitihada zinazofanywa katika sekta ya elimu
hasa katika masuala ya lishe kwa wanafunzi mashuleni katika kukabiliana
na tatizo la utapiamlo.
"Hii itasaidia kuleta
hamasa kuwaandaa watoto kwa kuwapatia lishe Bora ambayo itawasaidia
kufanya vizuri katika maisha yao,"Alisema.
Kwa upande wake mmoja wa
waumini wa kanisa hilo Bi, Naomi Nzota amesema waumini wa Jimbo la Njombe
wamefurahi Sana kwa kupata Askofu Dkt. Eusebius Kyando baada ya Misa wa
kuweka wakfu iliyoongozwa na Muasham Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dar es salaam
Polcapy Pengo.
"Ameueleza utumishi wa Askofu
Dkt. Eusebius Kyando kwamba ni mtumishi, mnyenyekevu mnyoofu na
mvumilivu," alieleza
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.