Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amepongeza taasisi ya Sukos Kova Foundation na taasisi ya Peaceland Foundation kwa pamoja kwa kushirikiana taasisi za uokoaji Serikalini kwa kuandaa mafunzo maalumu ya uokoaji kwenye maji.
Ametoa pongezi hizo wakati wa
hafla ya kufungua mafunzo hayo yaliyohusisha vikosi vya Jeshi la Polisi
Wanamaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na vikundi mbalimbali vya uokoaji
katika ngazi ya jamii iliyofanyika Sawasawa Bay Mikocheni,
Dar es salaam.
Amesema boti iliyokabidhiwa
Ofisi ya Waziri Mkuu itaenda kwenye maziwa mito na maeneo mbalimbali ili
ikakutane na taasisi za uokoaji na vikundi vya jamii ambavyo vitakuwa tayari
kwa mafunzo.
Waziri Mhagama amesema,
“maamuzi hayo ni ya kizalendo na tutaendelea kuheshimu uwepo wa taasisi hizo
binafsi, ikiwa ni pamoja na utaratibu ambao zitakuwa zimejiwekea katika kuleta
tija kubwa kwa taifa na ustawi wa Watanzania.”
Aliongezea kuwa matumizi ya
uokoaji yanaenda sambamba na matumizi ya vifaa hivyo na kutoa wito juu ya
utoaji wa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vifaa, kwa wakati sahihi na mahali
sahihi pale ambapo vitahitajika ili viweze kukabiliana na maafa pindi
yanapotokea.
"Boti iliyokabidhiwa ni
boti ya kisasa na kwa sababu mambo ya uokoaji ni mambo mtambuka yataenda
sambamba na uzuiaji wa uhalifu, na inaweza kutumika pia kuzuia uhalifu kwenye
maeneo ya maji katika Taifa letu.”alisema Mhe. Mhagama
Ofisi ya Waziri Mkuu
itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za kiraia ili kuweza kufika maeneo
mbalimbali yenye uhitaji wa kupata mafunzo ya uokoaji.
Aidha alitoa rai kwa taasisi
za uokoaji na vikundi vya uokoaji kuhakikisha wanatunza vifaa vilivyotolewa ili
viweze kudumu kwa muda mrefu huku vikiendelea kutoa msaada wa uokoaji .
Watakaopokea mafunzo watumie
vizuri maarifa hayo ili waweze kufunza wengine na kusaidia kundi kubwa kunufaika na mafunzo hayo ambayo yatatolewa
kwa muda wa wiki mbili, alisistiza
Waziri amesema, “ni vyema
taasisi za uokoaji na vikundi vya uokoaji vikatumia elimu itakayotolewa kwa
uzalendo mkubwa pindi tutakapokutana na majanga ya maafa.”
Waziri Mhagama alizikumbusha
taasisi Sukos Kova Foundation kuendelea kufungua milango ili taasisi nyingine
ambazo zinapenda kufanya ushirikiano na taasisi hiyo kwenye masuala ya uokoaji
wawe tayari kushirikiana.
Kwa upande wake Katibu Tawala
wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt, Koba Nguvila amesema Mkoa wa Dar es salaam
unaguswa kwenye habari ya uokoaji na mafaa kwa sababu Mkoa huo unapata mafuriko
na madhila ya kuchafuka kwa bahari.
Amesema kuwa hili ni jambo la
faraja kwa taifa, pindi inapotokea jamii imezungukwa na maji unatumia vifaa vya
kisasa vya uokoaji hivyo kusaidia kuimarisha usalama wa kuokoa watu.
Naye Kamishna Mstaafu Suleiman
Kova, amesema ya Sukos Kova Foundation kwa kushirikiana taasisi ya Peaceland
Foundation wametoa boti Moja ili liweze kuogeza nguvu katika miundombinu
iliyopo kazini.
"Tumeona tumpatie Jaketi
la Uokoaji (Life JacketRais) Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa sababu amekuwa
mstari wa mbele kutoa maelekezo makubwa wakati Maafa yanapotokea," alisema
Awali Mkuu wa Wajumbe kutoka Peaceland Foundation Bi. Jing
Ping, amesema nchi ya China na Tanzania wamekuwa na ushirikiano na mshikamano
wa karibu kwa zaidi ya miongo sita sasa.
"Nchi zetu zimekuwa
zikisaidiana katika mambo mbalimbali na tukio la leo ni moja ya ushahidi wa
ushirikiano wetu, na katika hili taasisi yangu kwa kushirikiana na Sukos Kova
Foundation zimejikita katika kuimarisha juhudi za kukabiliana maafa kwa kutoa
vifaa mbalimbali vya kusaidia uokoaji.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.