Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amewapongeza SUMA JKT kwa
hatua nzuri waliyofikia katika Ujenzi wa Nyumba za Makazi kwa wananchi
waliokumbwa na Mafuriko ya Mawe na Matope mwezi Disemba Mwaka Jana.
Waziri ametoa Kauli hiyo
wakati alipotembelea na kujionea maendeleo ya Ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa
katika eneo la Waret, katika Kijijiji cha Gidagamowd kata ya Mogitu wilaya ya
Hanang’.
Ujenzi wa nyumba hizi ni kielelezo
cha dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uzalendo kwa Taifa lake, utu
na mapenzi kwa wananchi katika kuwatumikia.
“Nimefurahi mmerithisha ujuzi
wa ujenzi kwa sababu nyumba hizi zimejengwa kwa ubora wa hali ya juu na kuzingatia
kanuni za kiuhandisi wakati wa ujenzi,” alisema Waziri Mhagama.
Aidha ameelekeza kwa uongozi
wa Mkoa wa Manyara kuhakikisha miundo mbinu ya Elimu, Soko na Afya inakamilika
kwa muda unaotakiwa kama ilivyofanywa katika urejeshaji wa hali kwa kuhakikisha
huduma za maji, nishati ya umeme inapatikana sambamba na ufunguaji wa barabara.
Waziri Mhagama amesema, “Makazi
yanapendeza na baada ya muda Mji huu utakuwa Mkubwa sana na utakuwa Mji wa
kihistoria ni vyema tukaendelea kutuna mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya
tabia nchi.”
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Hanang’ Mhe. Halimish Issa Hazali amesema Waziri Mhagama ametembelea Nyumba
za SUMA JKT nyumba 73 na 1 UWT na ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi na pia
ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba 35 zinazosimamiwa shirika
la Msalaba Mwekundu.
Nimshukuru Mhe. Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na anaendelea kuifanya kwa
wananchi wa Hanang.
Awali Kaimu Kamanda wa Ujenzi
wa Nyumba Luteni Kanali Ashiraf Hassan amesema wamefarijika kwa ziara ya Waziri
Mhagama na wamejipanga kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na ubora
unaotakiwa.
“Hatuwezi kumuangusha Mhe.
Rais Samia Suluhu Hassan katika adhima yake ya kuhakikisha anawapatia wananchi
wa Hanang waliokumbwa na Mafuriko ya Matope na Mawe nyumba bora,” alisema Kaimu
Kamanda wa Ujenzi Luteni kanali Hassan.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.