Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa Wananchi
kujitokeza kujiandikisha na kuhakiki
kumbukumbu zao katika Daftari la kudumu la Mpiga Kura.
Waziri
ametoa kauli hiyo wakati alipomuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, leo katika ibada ya shukrani ya ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Mariamu Lituhi - wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma.
Amewaomba wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua au
kuchaguliwa kwa yeyote mwenye sifa za kushirikina na wananchi kuongoza,
kutosita kuomba kuchaguliwa.
Waziri amesema, “tuendelee kuiweka nchi yetu kwenye maombi, tumlilie
Mungu tuvuke salama kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na tuvuke salama
kwenye Uchaguzi Mkuu ili Tanzania iendelee kubaki kuwa kisiwa cha Amani.”
Ameongeza kusema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatambua
mchango wa Kanisa Anglikana Tanzania katika Maendeleo ya Taifa letu Kiuchumi,
Kisiasa na Kijamii.
Aidha Waziri Mhagama ametumia tafakari
ya ujumbe wa Mungu kupitia kinywa cha Nabii Hagai sura ya kwanza, aya ya nane
(Hagai 1:8) aliposema, “Sasa, basi, nendeni milimani mkalete miti, mlijenge
upya hilo hekalu, nipate kulifurahia na kutukuzwa”.
Awali
katika taarifa ya risala iliyosomwa na Bi, Shukrani Eliya Kilumbo alisema ujenzi wa kanisa
ulianza Mwaka 2011 na mpaka sasa kimetumika kiasi cha Millioni 84 na
inakadiriwa kiasi cha shilingi milioni 150 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi
wa kanisa la Anglikana la Mt. Mariamu.
Tunashukuru
taaisisi mbalimbali na watu wote ambao wako hapa kwa kazi hii kubwa ya kuitikia
wito wa Mwenyezi Mungu aliowaagiza kupitia ujumbe wa Mtume Paulo kwa wafilipi
4,8;9
Katika ibada
hiyo ya shukrani kiasi cha Milioni 52,300,000 kilikusanywa ikiwemo fedha
taslimu na ahadi zitakazosaidia katika ujenzi wa kanisa la Anglikana la Mt,
Mariamu Lituhi katika wilaya ya Nyasa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.