Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi la Sheria
Ndogo za Mwaka 2024 katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha sita cha Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimewasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.
Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi
wa Bunge Jijini Dodoma Leo ambapo amesema mafanikio ya Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yanatokana na ushirikiano ambao umekuwa
ukitolewa na Kamati ya Bunge ya Sheria ndogo.
“Naomba niwahakikishie kamati;
nimepokea jedwali hili na tutawasilisha kwa Wizara zinazohusika ili zije zilete
majibu, naomba tuendele kupata ushirikiano wakati wizara hizo zitakapokuja kuwasilisha,”
alisema Naibu Waziri Ummy.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.