Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amesema ujenzi unaoendelea wa tanki kubwa la kuhifadhia maji safi kutoka Ruvu unatarajia kukamilika mapema mwakani ambapo litasaidia kuondoa kero ya maji Jijini Dar es salaam.
Waziri ametoa kauli hiyo
alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi na kuzungumza na
wananchi wa Banguko katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es salaam.
Ameeleza ujenzi wa bwawa hilo
utanufaisha wananchi takribani 450000 hasa wa Jimbo la Ukonga na Segerea na
Mkandarasi ameshalipwa fedha zote hivyo mradi utakapokamilika wananchi wote
wataunganishwa na mtandao wa maji.
“Hivyo tutashuhudia kata saba
katika Jimbo la Ukonga zitakazoondokana na adhaa ya upatikanaji wa maji,” alisema
Waziri Lukuvi.
Aidha tunashuhudia fedha
nyingi zinatolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji na barabara
na tumekubaliana usanishaji wa mikataba ufanyike katika maeneo husika ya ujenzi
wa miradi.
Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo
ni hatua lakini sisi tumekwenda kasi sana katika utekelezaji wake hivyo wananchi
mukiona vinaelea vimeundwa,
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Mhe, Albert Chalamila amesema Mkoa umejikita sana katika
kulinda amani na kuendelea kulinda raia na mali zao, ili wananchi waweze
kujikita katika shughuli za uzalishaji.
“Mwenyeviti wa Serikali za Mitaa
na kamati za ulinzi kwa kushirikisha na polisi jamiii, hakikisheni Madhila ya
wananchi kuogopa wahalifu yanadhibitiwa katika maeneo yenu,“ alisema Mkuu wa
Mkoa Chalamila.
Awali Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.
Edward Mpogolo amesema Serikali imejenga madarasa ya ghorofa zaidi ya 80 na
madarasa ya kawaida 465 kwa shule za sekondari, na kwa upande wa shule za
msingi madarasa zaidi ya 437 yamejengwa.
“Mafanikio haya yanakuja
kutokana na mahusiano tuliyonayao na wawakiishi wa wananchi wanaochagiza kwa
kiasi kikubwa maendeleo ya miradi ya maendeleo,” alisema Mkuu wa wilaya
Mpogolo.
Ikumbukwe katika ziara hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi,
alizindua Mradi wa Barabara ya Tukuyu Ilala na Kuweka Jiwe la Msingi katika
sekondari Liwiti.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.