Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi amesema Serikali itaendelea kuheshimu
misingi iliyowekwa na vyama vya siasa katika kujenga amani na
utulivu kwa watanzania wote.
Kauli hiyo ameitoa Jijini Dar
es Salaam katika ziara yake ya kutembelea Makao Makuu ya Ofisi za Vyama vya
UDP, NCCR MAGEUZI, CUF na NLD ambapo amepata nafasi ya kukutana na kufanya
mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Vyama hivyo.
Ameeleza kwamba tangu mfumo wa
vyama vingi umeanza nchini Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Chama Tawala vimekuwa
mhimili wa kujenga amani na umoja, hivyo
nawapongeza kwa kazi nzuri ya uzalendo mnayofanya.
“Niombe Viongozi wa Vyama
mhimize wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha ndani ya demokrasia ya vyama mnaweka wagombea ili
washindane na vyama vingine kupata viongozi,” alisema Waziri Lukuvi
Aidha Serikali itahakikisha
matangazo yote ya vijiji yanawekwa kwenye tovouti za Serikali ili wananchi
wafahamu vijiji, vitongoji na mitaa inayogombaniwa katika uchaguzi wa Serikali
za Mitaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
chama cha (UDP) Mhe. John Cheyo amemshukuru Waziri wa Nchi kwa kufanya ziara
katika Ofisi za Makao Makuu ya Vyama kwa sababu imeonesha dhamira ya dhati ya Serikali
katika kutekeleza falsafa ya 4R.
Mhe. Cheyo amesema “sisi kama
wadau wa siasa tunataka kushiriki katika kuona nchi inatawalika kwa amani na
kuchagiza maendeleo makubwa”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.