Mkurugenzi wa Idara ya Sera na
Uratibu wa Shughuli za Serikali, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na
Uratibu Bw. Paul Sangawe ameongoza Kikao cha Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa
wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), wakurugenzi wa sekta zinazotekeleza Programu ya
Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge na Uratibu pamoja na timu ya wataalamu.
Pamoja na mambo mengine kikao
hicho pia kimehusu mapitio ya Mipango na Bajeti ya Programu kwa kipindi cha
miaka minne ya utekelezaji iliyobakia.
Kikao hicho kimefanyika Zanzibar, katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.