Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy
Nderiananga amewashukuru wadau kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross
Tanzania) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kwa kutoa
misaada ya vifaa saidizi kwa ajili ya kuendelea kusaidia katika zoezi la
uokoaji linaloendelea kufuatia janga la kuporomoka jengo la ghorofa eneo la
Congo na Mchikichi Kariakoo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Ametoa shukrani hizo hii leo na
kueleza kuwa miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na machela tisa (9)
mashuka 100 kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) Pamoja na
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA, reflectors pamoja na cover white.
Naibu Waziri huyo ameendelea kutoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchangia huku akipongeza namna zoezi la uokoaji linavyoendelea kwa kushirikiana na wadau.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.