Mawaziri wa kisekta
wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.
William Lukuvi Leo Novemba 17,2024 wamekutana kwa ajili ya kuendelea na zoezi
la uokoaji wa watu waliokwama kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo kwenye mtaa
wa Congo na Mchikichi Jijini Dar es Salaam.
Mawaziri hao ni pamoja na Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godfrey
Mollel, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Mhe. Mwanaidi Khamis na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na
Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.