TANZANIA imeendelea kutolewa
mfano wa kuwa na Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura
(National Emergency Operation and Communication Center Situation Room) na
kuelezwa kuwa nchi nyingine ziendelee kuiga mfano wa Tanzania na kuendelea kuwekeza
katika mifumo ya tahadhali za mapema -early warning systems kwa kutumia vyanzo
vya ndani, kushirikisha jamii na sekta binafsi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi
ameyasema hayo 13 Novemba, 2024 wakati wa Mkutano wa 29 wa nchi Wanachama wa
Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaoendelea
mjini Baku, nchini Azerbaijan.
Dkt. Yonazi amesema
kuwa,Tanzania imeendelea kuwa kinara katika masuala ya menejimenti ya maafa
hususan katika kuzuia, kupunguza kujiandaa na kukabili maafa pindi yanapotokea,
huku akitaja mafanikio ya uwepo wa kituo cha ufuatiliaji wa majanga (situation
room) ikiwemo ya kurahisisha ufuatiliaji wa mwenendo wa janga lililotabiriwa na
kufanya uchambuzi wa kiwango cha madhara kwa jamii, miundombinu na mazingira.
Pia kituo hicho kimesaidia
kuandaa taarifa za tahadhari ya mapema ya hatua za kuchukua ili kuzuia,
kujiandaa na kukabili maafa, kuandaa taarifa ya mwenendo wa tukio na kusambaza
kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kusaidia uratibu na utekelezaji wa shughuli
za kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea.
Aidha alitumia fursa hiyo
kuwahamasisha wadau kuwezesha utekelezaji wa afua za usimamizi wa maafa katika
eneo la mifumo ya tahadhali ya mapema.
Dkt. Yonazi ametumia jukwaa
hilo kuyakaribisha Mataifa mbalimbali kuja kujifunza Tanzania namna Kituo hicho
kinavyofanya kazi katika kuratibu mwenendo wa majanga kwa umahiri wa hali ya
juu.
“Uwepo wa kituo hiki
umewavutia wadau wengi kuja kujifunza huku wengine wakiahidi kuunga mkono
juhudi za Tanzania katika masuala ya menejimenti ya maafa,” alisema Dkt. Yonazi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.