Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Utengamao cha Taifa unaotekelezwa na Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) katika eneo la Itega, jijini Dodoma.
Ziara
hiyo imefanyika leo na kuongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.
Edwin Swale (Mb) ikiwa ni sehemu ya majukumu ya kamati ya kusimamia na kukagua
utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mhe. Swale amesema kuwa kamati imeridhishwa na hatua ya
utekelezaji ambayo mradi umefikia kwani
unaenda kutimiza dhamira ya Serikali ya
Awamu ya Sita ya kujali Utu na Ustawi wa Watanzania.
Sambamba
na hilo, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu
kupitia Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za Kulevya kwa kubuni mbinu
ya jinsi ya kusaidia waraibu watokanao na matumizi ya madawa za kulevya.
Awali,Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy
Nderiananga amesema kuwa Mradi huo ni endelevu ikiwa ni juhudi ya Serikali
katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya na kuahidi kuendelea kushirikiana na
Taasisi binafsi katika mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya Nchini.

.jpeg)









