NA MWANDISHI WETU
Mnamo
mwezi Juni, mwaka 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa alitoa taarifa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli, ameagiza) fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kumbukumbu
ya siku ya Mashujaa kiasi cha Shilingi milioni 308, zitumike kuboresha
miundombinu ya barabara jijini Dodoma.
Kufuatia
agizo hilo, Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), walipata kiasi cha Shilingi
milioni 288 kwa ajili kuweka taa 57 kwenye barabara ya Emmaus-African Dream na
taa 42 kwenye barabara ya Kisasa. kiasi cha shilingi milioni 20 walipewa Wakala
wa Barabara Dodoma (TANROADS), kwa ajili ya kuhamisha taa ya kuongoza magari
kutoka njia panda ya Area D na kuwekwa kwenye makutano ya barabara ya Emmaus.
Tayari
TARURA wameanza kutekeleza agizo hilo kwa kuweka taa kwenye barabara ya Kisasa
na Emmaus-African Dream. Kwa upande wa TANROADS-Dodoma, zoezi la kuhamisha taa
ya kuongoza magari limetekelezwa, ambapo wakandarasi watakabidhi kazi hizo rasmi
mwezi Agosti mwaka huu.
Akiongea
wakati wa ukaguzi wa kazi hiyo katika barabara ya Emmaus-African Dream Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora
alifafanua kuwa, kuwekwa kwa taa kwenye barabara hizo ni utekelezaji wa agizo
la Mhe. Rais aliyetaka miundombinu ya barabara jijini Dodoma kuboreshwa, hali inayoongeza
usalama kwa watumiaji wa barabara hizo pamoja na kupandisha hadhi ya jiji na
makazi ya maeneo husika.
“Taa hizi ni za kisasa na zitasaidia uhifadhi wa
mazingira kwakuwa zinatumia mwanga wa jua, Serikali inajitahidi kuboresha
miundo mbinu ikiwemo barabara hii, hivyo wananchi ambao barabara inapita katika
makazi yao hawanabudi kuilinda miundombinu ya taa hizi. Fedha za walipakodi
zimetumika hapa itasikitisha kuona miundo mbinu ya taa hizi kukuta imeharibiwa”
amesisitiza Kamuzora.
Awali,
akielezea shughuli zinazoendelea katika barabara ya Emmaus-African Dream,
Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Dodoma,
Mhandisi Lusako Kilembe alibainisha kuwa taa hizo ni za kisasa na zina uwezo wa
kuhifadhi umeme hivyo zitasaidia kupunguza ghrama za uendeshaji na uhakika
katika matumizi ya barabara hizo.
Kampuni
ya Mionzi Jua Ltd ndiyo inayofanya kazi ya kuweka taa katika barabara za Kisasa
na Emmaus-African Dream, ambapo jumla ya kiasi cha Shilingi milioni 287.1 zitatumika
kukamilisha kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.