Na. OWM, DAR ES SALAAM
Wataalam wa TEHAMA kutoka
katika sekta za Afya ya Binadamu na Wanyama, wemepata mafunzo juu ya matumizi ya Programu (Software)
ya Kufanya uchambuzi wa Mtandao na Miundombinu ya Maabara (Laboratory
Infrastructure and Network Analysis), kwa kuzingatia Dhana ya Afya moja.
Mafunzo hayo yamefanyika
Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe, 6 hadi 7, Mei, 2019, ambapo washiriki
wameweza kufundishwa Programu ya LINA inavyojikita
katika kuwezesha Wataalamu wa Maabara na
watakwimu katika sekta ya Maabara wa sekta zote za Afya kuwa na uwezo wa
kuainisha maabara na uwezo wake wa kupima, ukusanyaji na utunzaji wa Takwimu za
maabara.
Matarajio ya matumizi ya Programu
hiyo katika maabara za hapa nchini ni kuwa itawezesha kuunda mtandao wa maabara za sekta
zote za Afya utakao wezesha utendaji kazi wa maabara hizo kuwa wa ufanisi na wa
wakati, kwa kuwa itawezesha kuainisha maabara zilizopo hapa nchini,
usafirishaji wa sampuli za vimelea na uhifadhi wa takwimu za matokeo ya vipimo
vya maabara hizo.
Kufanyika kwa mafunzo hayo kunachangia katika kutekeleza Agenda ya Usalama wa Afya Duniani
(Global Health Security Agenda - GHSA), Kanuni za Afya za Kimataifa (International
Health Regulations - IHR), Mpango wa Taifa wa Usalama wa Afya (National Action
Plan for Health Security), Mpango
Mkakakti wa Afya Moja (National One
Health Strategic Plan) pamoja na ujenzi wa usalama wa afya za wananchi wa hapa
nchini.
Mafunzo
hayo, yamewahusisha wataalamu wa TEHAMA kutoka sekta zote za Afya, wataalam wa
Afya ya Binadamu na Mifugo na yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Dawati la Uratibu wa Afya Moja kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Defense
Threat Reduction Agency (DTRA) na Sandia
National Labs.
MWISHO
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.