Wednesday, May 22, 2019

WATAALAMU WA TEHAMA WAPIGWA MSASA JINSI YA KUITUMIA PROGRAMU YA LINA KWA DHANA YA AFYA MOJA

Mtaalamu wa Programu ya LINA, Kutoka SANDIA National Labaratory, Patrick Finley akiwaeleza wataalam wa TEHAMA, wataalam wa sekta ya Afya ya Binadamu na Mifugo juu ya mtumizi ya Programu hiyo, wakati wa mafunzo ya kutumia Programu hiyo Jijini Dar es salaam,  Mei, 2019.
Na. OWM, DAR ES SALAAM

Wataalam wa TEHAMA kutoka katika sekta za Afya ya Binadamu na Wanyama, wemepata  mafunzo juu ya matumizi ya Programu (Software) ya Kufanya uchambuzi wa Mtandao na Miundombinu ya Maabara (Laboratory Infrastructure and Network Analysis), kwa kuzingatia Dhana ya Afya moja.

Mafunzo hayo yamefanyika Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe, 6 hadi 7, Mei, 2019, ambapo washiriki wameweza kufundishwa  Programu ya LINA inavyojikita katika kuwezesha Wataalamu wa  Maabara na watakwimu katika sekta ya Maabara wa sekta zote za Afya kuwa na uwezo wa kuainisha maabara na uwezo wake wa kupima, ukusanyaji na utunzaji wa Takwimu za maabara.

Matarajio ya matumizi ya Programu hiyo katika maabara za hapa nchini ni kuwa  itawezesha kuunda mtandao wa maabara za sekta zote za Afya utakao wezesha utendaji kazi wa maabara hizo kuwa wa ufanisi na wa wakati, kwa kuwa itawezesha kuainisha maabara zilizopo hapa nchini, usafirishaji wa sampuli za vimelea na uhifadhi wa takwimu za matokeo ya vipimo vya maabara hizo.

Kufanyika kwa mafunzo hayo kunachangia katika  kutekeleza Agenda ya Usalama wa Afya Duniani (Global Health Security Agenda - GHSA), Kanuni za Afya za Kimataifa (International Health  Regulations  - IHR), Mpango  wa Taifa wa Usalama wa Afya (National Action Plan for Health Security),  Mpango Mkakakti wa Afya Moja  (National One Health Strategic Plan)  pamoja na  ujenzi wa usalama wa afya za wananchi wa hapa nchini.

Mafunzo hayo, yamewahusisha wataalamu wa TEHAMA kutoka sekta zote za Afya, wataalam wa Afya ya Binadamu na Mifugo na  yameratibiwa na Ofisi ya Waziri  Mkuu, Dawati la Uratibu wa Afya Moja kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Defense Threat Reduction Agency (DTRA)  na Sandia National Labs.

MWISHO

Mtaalamu wa Programu ya LINA, Kutoka SANDIA National Labaratory, Walter Beyeler akiwaeleza wataalam wa TEHAMA, wataalam wa sekta ya Afya ya Binadamu na Mifugo juu ya mtumizi ya Programu hiyo, wakati wa mafunzo ya kutumia Programu hiyo Jijini Dar es salaam, Mei, 2019.
Mtaalamu wa Programu ya LINA, Kutoka SANDIA National Labaratory, Laura Jones akiwaeleza waratibu wa Dawati la Afya Moja Ofisi ya Waziri Mkuu juu ya mtumizi ya Programu hiyo, wakati wa mafunzo ya kutumia Programu hiyo Jijini Dar es salaam,  Mei, 2019.
Washiriki na wawezeshaji wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo ya matumizi ya Programu (Software) ya Kufanya uchambuzi wa Mtandao na Miundombinu ya Maabara (Laboratory Infrastructure and Network Analysis), kwa kuzingatia Dhana ya Afya moja, yaliyofanyika   Jijini Dar es salaam,  Mei, 2019.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.