NA; MWANDISHI WETU
Serikali
ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta
ya usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi.
Akizungumza
Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Vyama vya
Madereva na Vyama vya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga
mazingira wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini
wakiwemo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.
“Moja
ya maazimio ya mkutano wetu wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri
ambao hawajatoa mikata ya ajira kwa madereva wao waanze kutoa mikataba ya ajira
iliyoboreshwa suala hilo lianze kutekelezwa mara moja kwa kuwa ni takwa la
kisheria na sio jambo la hiari” Alisisitiza Mhagama
Kutolewa
kwa mikataba hiyo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo
mwaka 2017 yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira iliyoboreshwa kwa madereva
wote itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande hizo na Taifa kwa ujumla.
Alifafanua
kuwa mkutano huo umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kati ya Serikali,
wamiliki na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo ili kuchochea ustawi wa
sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na mapungufu yaliyobainika katika
ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti 2019 kwa lengo la kuona namna sheria
za kazi zinavyozingatiwa.
Azimio
jingine ni kuendelea kutoa elimu kwa makundi hayo kupitia vyama vya wamiliki na
madereva ili kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo hasa zilizoibuliwa katika
ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Aidha,
Waziri Mhagama ameviagiza vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji
kuhakikisha wanaruhusu wafanyakazi kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi
kwa Makapuni ambayo hayajafanya hivyo bado.
“Vyama
vya wafanyakazi vinasaidia sana kuleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi
maana wafanyakazi hutumia vyombo hivyo kushauriana namna bora ya kutatua
changamoto zinazowakabili,” alisema Mhagama
Katika
hatua nyingine Waziri Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa vyombo hivyo
kuendelea kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima pande zote mbili, Serikali
itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi hiyo.
Kwa
upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira Mhe. Antony
Mavunde amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yatasaidia
kutatua changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya
usafirishaji.
Mkutano
wa wadau wa sekta ya usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma ukishirikisha Wizara
zinazohusika na masuala ya uckuzi na Ujenzi.
|
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la
shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa
sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama
vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika Novemba 1,
2019 Dodoma.
|
|
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista
Mhagama na Naibu wake Mhe Antony Mavunde wakishuhudia zoezi la utiaji saini wa
maazimio ya kikao cha pamoja kati ya wadau wa sekta ya uchukuzi na Serikali
kilichofanyika Novemnba 1, 2019 Jijini Dodoma.
|
|
Katibu
Mkuu wa TABOA Bw. Enea Mrutu akichangia jambo wakati wa Kikao cha majadiliano
kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya
madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.
|
|
Kaimu
Kamishana wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe
Andrew Mwalwisi akiwa katika kikao cha majadiliano kati ya Serikali na
wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi
wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.
|
|
Baadhi
ya washiriki wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya
usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya
wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA wakifuatilia hotuba ya Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Hayupo
pichani) wakati wa kikao hicho.
|
|
Viongozi
wa vyama vya wa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi
Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake
Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira,
Vijana na Wenye Ulemavu).
|
|
Viongozi
wa vyama vya wa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi
Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake
Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira,
Vijana na Wenye Ulemavu).
|
|
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la
shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa
sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama
vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika Novemba 1,
2019 Dodoma.
|
|
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.
Andrew Masawe akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha majadiliano
kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya
madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo
TABOA.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.