Friday, November 1, 2019

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA USAFIRISHAJI:WAZIRI MHAGAMA

 

NA; MWANDISHI WETU
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi.

Akizungumza Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Vyama vya Madereva na Vyama vya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini wakiwemo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

“Moja ya maazimio ya mkutano wetu wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawajatoa mikata ya ajira kwa madereva wao waanze kutoa mikataba ya ajira iliyoboreshwa suala hilo lianze kutekelezwa mara moja kwa kuwa ni takwa la kisheria na sio jambo la hiari” Alisisitiza Mhagama

Kutolewa kwa mikataba hiyo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mwaka 2017 yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira iliyoboreshwa kwa madereva wote itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande hizo na Taifa kwa ujumla.

Alifafanua kuwa mkutano huo umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kati ya Serikali, wamiliki na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo ili kuchochea ustawi wa sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti 2019 kwa lengo la kuona namna sheria za kazi  zinavyozingatiwa.

Azimio jingine ni kuendelea kutoa elimu kwa makundi hayo kupitia vyama vya wamiliki na madereva ili kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo hasa zilizoibuliwa katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Aidha, Waziri Mhagama ameviagiza vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha wanaruhusu wafanyakazi kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi kwa Makapuni ambayo hayajafanya hivyo bado.

“Vyama vya wafanyakazi vinasaidia sana kuleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi maana wafanyakazi hutumia vyombo hivyo kushauriana namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Mhagama 

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kuendelea kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima pande zote mbili, Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

Mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma ukishirikisha Wizara zinazohusika na masuala ya uckuzi na Ujenzi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika Novemba 1, 2019 Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama na Naibu wake Mhe Antony Mavunde wakishuhudia zoezi la utiaji saini wa maazimio ya kikao cha pamoja kati ya wadau wa sekta ya uchukuzi na Serikali kilichofanyika Novemnba 1, 2019 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa TABOA Bw. Enea Mrutu akichangia jambo wakati wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

Kaimu Kamishana wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Andrew Mwalwisi akiwa katika kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.
Viongozi wa vyama vya  wa wamiliki wa  vyombo vya usafirishaji  wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).
Viongozi wa vyama vya  wa wamiliki wa  vyombo vya usafirishaji  wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika Novemba 1, 2019 Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew  Masawe akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.



EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.