WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewashukuru watu wote waliojitokeza katika
mazishi ya kaka yake Mzee Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi
(Jumatatu, Novemba 04, 2019) nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila ‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.
Ametoa
shukrani hizo leo (Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya
mazishi iliyofanyika kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema
kwamba hayo ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia
hiyo.
“Tulikuwa
12 na sasa tumebaki watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba
huu kwetu ni mkubwa umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini
hatuna namna ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea
kumuombea. Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia,
familia imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.”
Waziri
Mkuu pia amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole
alizozitoa. “Jambo hili pia limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye
ametutaka tuwe watulivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja
kwa dhehebu lake aendelee kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze
mahala pema.”
Amesema alipata taarifa za msiba huo wakati akijiandaa kwenda wilayani Ruangwa kwa ajili ya kushiriki mazishi yamwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Kaspar Selemani Mmuya.
Kwa upande wake,
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Venance Mabeyo akitoa
salamu za pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi
na Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na majonzi waliyonayo
kwa kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kuwa ndiye anayetoa na anayetwaa. “Hakuna namna ya kurekebisha maamuzi
ya Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu kwa sala Mwenyezi
Mungu ampokee kwa amani.”
Naye,
Mwakilishi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo
amesema amewataka wananchi wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni
kawaida kwa binadamu kujisahau lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya
kutukumbusha juu ya uwepo wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale
yalikuwa ya wajibu kuyatekeleza.”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.