Wednesday, April 22, 2020
Tuesday, April 21, 2020
WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBI YA KITAIFA KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA
*Idadi ya wagonjwa yafikia 284, ataka tahadhari zaidi iongezwe
*Aomba viongozi wa dini wahakikishe mikusanyiko ibadani inapungua
*Akemea wanaopandisha bei za vyakula hasa sukari
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia jana (Aprili 21, 2020) jumla ya wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona (Covid-19) ambapo wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, saba wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 22, 2020) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini walioshiriki maombezi ya Kitaifa dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1,733 walikutwa hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284).
“Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa ifikapo mwishoni wa Aprili, 2020 nchi yetu ingekuwa na wagonjwa 524,716 lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa kadirio hilo hatujalifikia.”
Kuhusu hali ya maambukizi ilivyo nchini, Waziri Mkuu amesema Jiji la Dar es Saalam na kisiwa cha Zanzibar, yanaongoza kwa maambukizi na akataka tahadhari zaidi zichukuliwe. “Jiji la Dar es Salaam ndio lina maambukizi makubwa hivyo nawasihi wananchi kama huna jambo lolote la kufanya huna sababu ya kuzurura na kwa wafanyabiashara siyo lazima mje Kariakoo, unaweza kufanyia biashara katika eneo lako,” amesisitiza.
“Ni wakati kila mmoja kuendelea kuchukua tahadhari vya kutosha ili kuepuka maambukizi. Epuka misongamano isiyokuwa ya lazima, huna sababu ya kumuamini yeyote, ona kuwa kila mmoja ana ugonjwa.”
Kipekee, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini waendelee kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na ugonjwa huo kwa kuwaelimisha waumini wachukue tahadhari zote muhimu. “Ninawaomba viongozi wa dini wachukue tahadhari zaidi kwa kuhakikisha mikusanyiko kwenye nyumba za ibada inapungua ikiwemo waumini kukakaa kwa nafasi, umbali wa angalau mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine na kuweka maeneo ya kunawa kwa maji na sabuni pamoja na vitakasa mikono katika nyumba zote za ibada.
“Kupunguza idadi ya siku za kukutana kufanya ibada na masaa ya ibada au mahubiri kila inapobidi. Kwa mfano, mikutano au shughuli za mikusanyiko za vikundi vya uimbaji, vijana, akinamama au waumini kwa ujumla ni vema zikasitishwa katika kipindi hiki,” amesisitiza.
Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti kuenea zaidi kwa ugonjwa huu zikiwemo za kutoa elimu ya namna ya kujikinga, kuunda Kamati za Kitaifa kwa ngazi za Mawaziri, Makatibu Wakuu, Timu ya Wataalam wa afya pamoja na kutoa maelekezo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama.
“Tumetenga maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu, tumenunua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huu hususani kwa watoa huduma wa afya. Tumeimarisha maabara zetu kwa lengo la kupanua wigo wa kufanikisha upimaji wa sampuli, vituo zaidi ya saba nchini ambapo upimaji wa awali unaanzia huko na kwenda kuhakikishwa katika Maabara Kuu ya Taifa,” amesema.
Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetaja mikoa ambayo imepata wagonjwa wapya 30 kutoka idadi ya 254 iliyotangazwa mara ya mwisho.
Wagonjwa hao na idadi yao kwenye mabano wanatoka mikoa ya Dar es Salaam (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani (2), Dodoma (2). Mingine ni Kagera, Manyara na Morogoro ambayo yote ina mgonjwa mmoja mmoja.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaopenda kupandisha bei za vyakula wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Wiki hii waumini wa Kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan, hivyo natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu katika kipindi hiki vinauzwa kwa bei ya kawaida, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wafanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile.”
Amesema kuwa hivi sasa kuna sukari ya kutosha nchini hivyo bei itaendelea kuwa ileile bila kujali msimu. “Ninaawagiza Wakuu wa Mikoa, yeyote atakayekutwa anauza sukari kwa bei ya sh.4,500, chukua hatua dhidi yake kwani hayo si malengo ya Serikali yetu,” amesisitiza.
Kwa upande wao, wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa dini walioshiriki maombi hayo, wameipongeza Serikali kwa hatua ambazo imezichukua hadi sasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.
(mwisho)
Monday, April 20, 2020
MAENDELEO YA UBUNIFU WA MJI WA SERIKALI YAJADILIWA
Na. OWM, Dodoma.
Ofisi ya Waziri Mkuu
inaendelea na zoezi la kuratibu awamu ya pili ya uendelezaji wa mji wa serikali
eneo la Mtumba, makao makuu ya nchi jijini Dodoma. Awamu hii ya pili inahusisha
Ubunifu na ujenzi wa majengo makubwa ya Ofisi zitakazotumiwa na Wizara za
serikali.
Akiongea, leo tarehe
20 Aprili, 2020, katika kikao cha Kamati
ya Makatibu wakuu na Wataalamu wa michoro ya Ubunifu na usanifu wa majengo, Katibu Mkuu
ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge),Tixon Nzunda, amefafanua kuwa
awamu hii ya pili ya inajikita katika kuboresha ubunifu na usanifu
wa mji wa serikali, ulioko Mtumba, Jijini Dodoma.
Aidha, kufanikiwa kwa mpango huo kutachangiza jiji la Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa
linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma
hiyo, tayari Timu ya Wataalam imepitia michoro
ya ubunifu na usanifu. Pia Wakala wa majengo Tanzania (TBA), inaendelea kufanya
kazi kwa karibu na Taasisi nyingine
zinazohusika na miundo mbinu katika mji wa Serikali kama vile TARURA, DOWASA,
TANESCO, TPDC, TTCL na eGA.
Hivi karibuni , Mwezi Februari mwaka huu, 2020,
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizindua Mpango Kabambe wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo aliwataka wadau mbalimbali kutoa
ushirikiano kwa kiwango cha juu katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kulifanya kuwa jiji bora na la
kisasa nchini.
Serikali, kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kutekeleza zoezi la kuhamishia shughuli za
Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa zoezi hilo uanze mwezi Septemba 2016.
Uamuzi wa kuhamishia
shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama
cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa
awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
MWISHO.
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi
wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20,
Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri
Mkuu, Dodoma.
|
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi
wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20,
Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri
Mkuu, Dodoma.
|
Prof. John Lupala
akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Ubunifu wa mpango wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili
katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma wakati wa kikao kazi cha makatibu
Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020.
Friday, April 17, 2020
BUNGENI LEO 16.04.2020
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 16, 2020. |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2020/2021. |
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa Shamsi Vuai Nahodha, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 16, 2020. |
Wednesday, April 15, 2020
MAJALIWA AZUNGUMZA KWA NJIA YA VIDEO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA MWANZA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 15, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 15, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 15, 2020. |
Tuesday, April 14, 2020
WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA URATIBU WA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU (COVID - 19)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
SHULE ZOTE NA VYUO KUENDELEA KUFUNGWA – MAJALIWA
*Sherehe za Muungano, Mei Mosi zaahirishwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.
Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima, hivyo maeneo hayo yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia majumbani kwao.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameagiza sh. milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pia, Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema elimu ya tahadhari ni muhimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. “Kama si lazima kutoka, wananchi waendelee kutulia majumbani mwao.”
Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kusimamia utoaji wa elimu ya kujikinga na virusi hivyo hasa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ikifuatiwa na Zanziba. “Ni muhimu wananchi wake wakapewa tahadhari juu ya namna ya kijikinga.”
Waziri Mkuu ameagiza kuwa wataalamu wanaosimamia utoaji wa huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wa watu wenye maambukizi ya COVID-19, wakiwemo madaktari wote wapewe vifaa vya kijikinga ili kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huo.
Amesema watu waliokutana na wagonjwa waendelee kufuatiliwa kwa umakini na wahusika wawashirikishe viongozi wote hadi wa ngazi za chini na kwamba athari za kiuchumi zinazojitokeza kufuatia ugonjwa huo ziendelee kuchambuliwa.
Machi 17, 2020 na Machi 18, 2020, Serikali ilitangaza kuzifunga shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu kwa muda wa siku 30 na kwamba wanafuzi wa kidato cha sita waliopaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 nao wangepaswa kusubiri Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi.
Akitangaza uamuzi huo, Waziri Mkuu pia alisisitiza kuwa mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo ya lazima imesitishwa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli nyingine za kijamii.
Alizitaka wizara na taasisi zizitishe semina, warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini ambayo inahusisha washiriki toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi makubwa, wanashauriwa wasitishe safari hizo,” alisisitiza.
Akielezea hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine.
BUNGENI 14.04.2020
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt, Mary Mwanjelwa, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Kijitoupele, Shamsi Vuai Nahodha, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
|
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mbunge wa Bukoba vijijini Jason Rweikiza, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, akichangia mada, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, akichangia mada, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akizungumza, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akizungumza, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. |
Monday, April 6, 2020
BUNGE LA BAJETI 06.04.2020
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati alipohitimisha hoja kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 6, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati alipohitimisha hoja kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 6, 2020. |
MAJALIWA AZUNGUMZA KWA NJIA YA VIDEO NA WAKUU WA MIKOA YA MIPAKANI.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya mipakani kuhusu ugonjwa wa Corona akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 6, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya mipakani kuhusu ugonjwa wa Corona akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 6, 2020. |
WAZIRI MKUU: WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 24, WATATU WAMEPONA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
hadi leo, hapa nchini kuna wagonjwa
24 waliothibitika kuwa na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) ambapo
watatu kati yao, wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitali, mmoja amefariki dunia
na wagonjwa 20 wanaendelea vema na matibabu.
“Serikali
imeendelea kuwafuatilia watu 685 waliokutana na wagonjwa hao ambapo watu 289
wamemaliza siku 14 za kufuatiliwa na vipimo vyao vimethibitisha kuwa hawana
maambukizi ya virusi vya Corona. Watu wengine 396 waliobaki wanaendelea
kufuatiliwa ili kujiridhisha iwapo hawana maambukizi ya virusi hivyo.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 6, 2019) Bungeni jijini Dodoma kwenye
mkutano wa 19 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi
zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2020/2021.
Amesema
hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona ni
pamoja na kufanya ukaguzi (screening) kwa wageni wote wanaoingia nchini kutoka nje
pamoja na kuwaweka katika uangalizi kwa siku 14.
“Ndege
zetu tumezuia kufanya safari za nje, tumezuia wafanyakazi kwenda nje ya nchi,
tumeimarisha mipaka sambamba na kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini
wanalazimika kuwekwa chini ya uangalizi wa lazima kwa siku 14 kwa lengo la kudhibiti
mienendo ya wasafiri chini ya ulinzi wa masaa 24,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema kutokana na umuhimu wa kuwatenga watu wanaofuatiliwa,
Serikali imeagiza mikoa yote nchini itenge maeneo maalumu kwa ajili ya
uangalizi na kujiridhisha iwapo hawana maambukizi.
“Hatua
hii ni muhimu katika kudhibiti kuenea zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Kayi ya hao, wengi ni wale waliotoka nje ya nchi. Maeneo hayo yametengwa kwa nia
njema na yako kwa viwango tofauti kulingana na uwezo wa kifedha wa wahusika.
Yako mabweni, ziko nyumba, na vyote vimewekwa kwa kuzingatia gharama mtu anayoweza
kumudu,” amesisitiza.
“Tunafanya
hivi ili kuondoa manung’uniko yaliyokuwepo kwamba watu wanapelekewa katika
maeneo ambayo hawawezi kumudu. Na baada ya kuchukua hatua hizo, sasa hivi
malalamiko hayo yamepungua.”
Akielezea
hatua mbalimbali ambazo zinachukuliwa hivi sasa, Waziri Mkuu amesema Serikali
inaimarisha maabara mbalimbali nchini ili ziweze kutoa huduma za upimaji ikiwemo
maabara zilizopo kwenye mikoa ya Arusha, Dodoma Kigoma, Mbeya, Morogoro,
Mwanza, Pwani na Tanga.
“Hospitali
za Rufaa za Kanda na Mikoa nazo zinaratibiwa kutoa huduma ya upimaji sambamba
na maeneo ya mipakani. Shughuli hizo za upimaji zinafanyika kwa usimamizi wa
Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii kwa lengo la kuthibitisha ubora wa vipimo
hivyo na kuratibu utoaji wa matokeo.”
“Nilishasema
atakayetoa taarifa za ugonjwa ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, na kama itabidi nitatoa mimi mwenyewe na kama italazimika sana
atatoa Makamu wa Rais au Mheshimiwa Rais mwenyewe. Hii hali ya Wakuu wa mikoa
na Wilaya kutoa matamko kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge hapa, haiku sawa.”
Waziri
Mkuu amesema Tanzania imeendelea kushirikiana kwa
karibu na Shirika la Afya Duniani (WHO), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuweka mikakati ya
pamoja ya kuimarisha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu
(COVID-19) na kwamba itaendelea kufanya tathmini kuhusu changamoto zinazoweza
kusababishwa na ugonjwa huo na namna ya kuzitatua.
Bunge
lilikubali kupitisha sh. 312,802,520,000 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi
zilizo chini yake kwa mwaka 2020/2021. Kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000
ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya matumizi
ya maendeleo.
Vilevile,
Bunge liliidhinisha sh. 121,786,257,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati
ya hizo, sh. 113,567,647,000 ni za matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
MAJALIWA: WAGONJWA WAWILI WA CORONA WAONGEZEKA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema jana (5 Aprili, 2020) wagonjwa wawili wa
corona wameongezeka, hivyo Tanzania ina jumla ya watu 22
waliothibitishwa kuwa na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi
vya corona (COVID-19) na kwamba wote wanaendelea vizuri.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa waimarishe ulinzi kwenye
vituo vyote vilivyotengwa kwa ajili ya kuwaweka watu wote wanaoingia
nchini na wahakikishe hakuna anayetoka ili kuepuka kusambaa kwa virusi
vya corona.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatatu, Aprili 6, 2020) wakati
akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Kamati zao za Ulinzi na Usalama za
Mikoa ya Mipakani ya Arusha, Rukwa, Katavi, Dar Es Salaam, Tanga,
Mtwara, Mara, Pwani, Ruvuma, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Kagera, Kigoma
na Songwe.
Waziri
Mkuu amesema kati ya wagonjwa hao 12 wapo mkoani Dar Es Salaam,
wagonjwa saba wapo Visiwani Zanzibar, Mkoani Kagera kuna mgonjwa mmoja
na mkoani Arusha kuna wagonjwa wawili na kwamba Serikali inaendelea
kupokea sampuli za vipimo kutoka kwenye mikoa mbalimbali.
“Wagonjwa
hawa wote ni wale waliotoka katika nchi mbalimbali, hivyo Wakuu wa
Mikoa mnawajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya
kujikinga na virusi vya corona hususani katika maeneo yanye
mikusanyiko.”
Waziri
Mkuu amewataka viongozi hao waendelee kuimarisha ulinzi katika maeneo
ya mipakani, viwanja vya ndege, bandarini na wahakikishe wageni wote
wanaoingia nchini wanapelekwa kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa kwajili
ya kuangaliwa kama wanamaambukizi ya COVID-19.
Pia,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa
wasimamie na wahakikishe watoa huduma katika maeneo hayo wakiwemo
walinzi wanapatiwa vifaa kwa ajili ya kujikinga ili wafanye kazi zao
bila ya kuwa na mashaka.
“Imarisheni
vituo na simamieni watu wasitoke kwenda mitaani na lazima washirikiane
ili maambukizi yasizidi kusambaa nchini. Fuatilieni historia za watu
wanaoingia nchini kuona maeneo waliyotembelea katika kipindi cha siku 14
kabla ya kuingia nchini.”
Kwa
upande wao Wakuu hao wa Mikoa wamesema wanaendelea kutekeleza maelekezo
yote yaliyotolewa na Serikali kuhusu namna ya kukabiliana na virusi vya
corona na kuhakikisha havisambai
zaidi nchini.