Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mhe. Zubeir Maulid ameipongeza kazi kubwa iliyofanywa na Serikali na
Wananchi waliojitolea kusaidia Waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe na
tope kutoka Mlima Hanang’ mkoani Manyara.
Ametoa kauli hiyo alipongoza
ujumbe kutoka baraza la wawakilishi kutoa Msaada wa kibinadamu kwa waathirika
wa maporomoko hayo katika Halmashauri ya wilaya ya hanang yaliyotokea Disemba
3, 2023.
Alieleza kwamba, jambo hili
limeonesha kiasi gani nchi yetu ina umoja hususan tunapopata matatizo na namna
gani tunashirikiana kama ndugu kulitatua.
“Tumekuja tumeleta kiasi cha
shilingi milllioni 30 tunajua mahitaji ni makubwa lakini kidogo kidogo,
tukiunganisha nguvu zetu jambo litakuwa kubwa ili isaidie waathirika,
“alibainisha.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amewashukuru,
baraza la wawakilishi kwa msaada wa kibinadamu walioutoa kwa waathirika.
“Jambo hili limeonesha kwamba
Muungano wetu si Muungano wa maneno bali ni Muungano wa vitendo,” alifafanua Waziri Mhagama
Aliongezea kuwa Serikali
itaendelea kuratibu vyema suala hilo na kuhakikisha kila mchango unatumika kwa
lengo lililokusudiwa na si vinginevyo na kuongezea kwamba watadhibiti kila
mianya ya ubadhilifu na kusisitiza kuwa kwa yeyote atakayefuja michango hiyo
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.