Imeelezwa kwamba hali ya amani
utulivu na ushirikiano unaosimamiwa na Viongozi Wakuu wa Nchi imesaidia katika
kuleta chachu kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Tanzania Bara na
Tanzania Visiwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera
Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi ametoa kauli hiyo leo wakati wa
hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika
ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Mkoani ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Amefafanua kwamba uongozi wao
bora; hatuna budi kuendelea kuwaombea viongozi wetu, kila mmoja kwa dini yake
ili Mwenyezi Mungu awape afya na nguvu ya kuendelea kutuongoza kwa mshikamano.
Waziri Lukuvi amesema, “chini
ya uongozi wao Tanzania Bara imetulia na Tanzania Visiwani imetulia na hivyo
kuwezesha haya kufanyika na kuendelea kuchochea maendeleo makubwa, mwenye macho
haambiwi tazama.”
Sote ni mshahidi
wa hatua kubwa za maendeleo zinazoendelea kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kupitia uongozi wa awamu ya nane chini ya Mhe. Daktari Hussein Ali
Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Waziri Lukuvi
amesema, mafanikio ya Serikali ya awamu ya nane yanaonekana wazi katika nyanja
za siasa na utawala bora, uchumi, huduma za kijamii na namna utamaduni wa watu
wa Visiwa vya Zanzibar unavyoenziwa na kuheshimika wakati wote.
Aidha Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar imechukua hatua za makusudi kuja na mradi wa ujenzi wa jengo
hili la Mahakama ya Wilaya pamoja na majengo mengine ya Mahakama za Mikoa na
Wilaya kule Unguja na hapa Pemba ili kukabiliana na changamoto za miundombinu
ya majengo.
“Ujenzi wa jengo hili ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa
majengo saba ambao ulipangwa kufanyika katika mwaka wa fedha wa 2023/2024
alisema,” Waziri Lukuvi.
Kwa upande wake Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Jaji Mkuu wa Zanzibar amesema Rais. Mhe. Daktari Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewaheshimisha kwa kuwajengea majengo saba ya Mahakama za Mkoa na wilaya katika visiwa vyote vya unguja na pemba.
“Tumekusudia kusogeza
huduma kwa wananchi kwa kujenga mifumo imara ya usimamizi wa haki ili kuboresha
huduma zetu za mahakama kuwa za kisasa ,” alisema Mhe, Jaji, Khamis.
Naye Mhe,
Valentina Katema, Mrajis wa Mahakama
Kuu Zanzibar, amesema miundo mbinu ya majengo ya mahakama ipo katika muundo zamani
hivyo kusababisha kushindwa kuendesha shughuli zake katika mazingira ya kisasa.
”Ujenzi wa majengo mapya ya Mahakama itasaidia, kupunguza msongamano
wakati wa utoaji wa huduma na kusaidia wananchi kupewa huduma kwa kuendana
na mahitaji ya kisasa,” alisema Mrajis.