Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Dkt. Lembulung Lukumay
ameipongeza Serikali kwa kuwekeza fedha katika ujenzi wa miundombinu ya sekta
ya afya pamoja na uboreshaji wa upatikanaji vifaa tiba.
Dkt.
Lukumay ametoa pongezi hizo leo Jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya Muundo
na Majukumu ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) iliyo chini Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu.
“Serikali imeongeza idadi ya madaktari
wabobezi katika jitihada za kuboresha huduma za afya ikiwemo kuweka utaratibu
mzuri wa kuendelea kuwezesha afua za UKIMWI kwa kutegemea fedha zetu za ndani
ili kuendeleza upatikanaji wa dawa,” alieleza Dkt. Lukumay.
Aidha, amebainisha kuwa, wananchi hawana budi
kuelezwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais,
Dkt, Samia Suluhu Hassan katika uimarishaji wa huduma za afya, katika ngazi ya
Zahanati, Vituo vya afya, hospitali za Wilaya na hospitali za Mikoa.


No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.