Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Damas Daniel
Ndumbaro, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye
Ulemavu) pamoja na taasisi zake kwa utendaji mzuri katika kuratibu shughuli za
Serikali zinazogusa maisha ya wananchi.
Pongezi
hizo zimetolewa leo jijini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya
utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Waziri Mkuu mbele ya Kamati hiyo ya Bunge.
Mhe.
Ndumbaro amesema maeneo ya uratibu wa maafa na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi
yanahitaji kuendelea kupewa kipaumbele ili Serikali iendelee kuwafikia wananchi
kwa ufanisi.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Ummy Nderiananga, amesema
Serikali imetenga fungu maalum la fedha kwa ajili ya afua za UKIMWI pamoja na
kushughulikia masuala ya maafa kila mwaka wa bajeti, hatua itakayohakikisha
utekelezaji endelevu wa majukumu hayo nchini.


No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.