Naibu
Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu),
Mhe. Ummy Nderiananga, amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwawezesha
kiuchumi watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya
Halmashauri, ikiwemo asilimia 2 inayotengwa mahsusi kwa kundi hilo.
Mhe.
Nderiananga ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha alipokutana na watu wenye
ulemavu ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake iliyoanza Wilaya ya
Moshi-Kilimanjaro.
Naibu
Waziri Nderiananga, amewapongeza watu wenye ulemavu wa Mkoa wa Arusha kwa
nidhamu ya kurejesha mikopo kwa wakati na kuhimiza waliomaliza kurejesha waweze
kuomba tena ili kupanua shughuli zao za kiuchumi.
Aidha,
ameelekeza kuwa 30% ya manunuzi ya umma kwenye Halmashauri zote za Jiji la
Arusha ziende kwenye makundi haya maalum kama vile watu wenye ulemavu,
“tunapotengeneza masoko tutenge maeneo
maalumu kwaaajili ya watu wenye ulemavu, na nataka kuona miradi ya watu wenye
ulemavu kuwa ni miradi ya kielelezo Nchini’’Mhe. Nderiananga amesema
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi ameishukuru
Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuwakwamua kiuchumi watu wenye
ulemavu, na ameahidi kuandaa hafla
kwaajili ya kuwapongeza wanufaika wa Mikopo ya 2% waliofanya vizuri ili iwe
kama sehemu ya hamasa na kielelezo kwa wale ambao hawajafanyi vizuri na ambao
wanatamani kupata mikopo hiyo.
Awali,
Mkurugenzi wa Idara ya watu wenye ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera
Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Bw. Kizito Wambura amesema Serikali inania
thabiti ya kuleta mabadiliko kwa watu wenye ulemavu na kutatua changamoto zilizobainishwa kupitia
mfumo wa kieletroniki wa taarifa za watu wenye ulemavu (PDMIS) ambao
tunategemea ufike kwenye maeneo yote ya Tanzania.

