Home
All posts
Wednesday, March 21, 2018
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi ameongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo na kuwaasa wajumbe wa baraza kutoa maoni yatakayosaidia kufanikisha mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2018/2019.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho Tarishi amesema kuwa Watumishi wote katika Ofisi hiyo wanao wajibu wakushiriki kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya bajeti ili kufanikisha azma ya Serikali kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Bila kujali nafasi zenu ni lazima mtambue kuwa mnao wajibu sawa katika kutoa maoni yatakayosaidia katika mchakato wa maandalizi ya bajeti” alisisitiza Bi. Tarishi.
Akifafanua Tarishi amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikizingatia maoni ya wajumbe wa baraza hilo katika maandalizi ya bajeti hivyo ni wakati mwingine tena kwa watumishi hao kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika kikao cha baraza hilo kwa kutoa mchango utakaosaidia katika utendaji wa Ofisi hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti.
Aliongeza kuwa Baraza hilo linafanyika ikiwa ni utekelzaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayotaka Ofisi zote za Serikali kuwapa nafasi watumishi wake kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo bajeti kupitia kwenye baraza la Wafanyakazi hali inayochochea maendeleo na tija katika utoaji wa huduma.
Naye Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma Bw. John Mchenya alieleza kuwa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanapaswa kuwa kielelezo katika uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu yao ili kuwa mfano wa kuigwa hususan katika kukilinda na kuhakikisha uhai wa chama cha Wafanyakazi kwa kutenda haki kwa mujibu wa sheria zilizopo.
“Ni vyema kila mmoja wenu akawa wakili mzuri katika utendaji kuzingatia Ofisi hii ndiyo mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali bila kuacha kuzingazita uwepo wa TUGHE kwa kuwa ipo kwa mujibu wa Sheria namba 6 inayoeleza masuala ya ajira na usajiri wa vyama vya Wafanyakazi”.Alisema Bw.Mchenya
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo Bw.Yona Mwakilembe amesema kuwa maoni ya watumishi katika Ofisi hiyo yamekuwa yakizingatiwa kwa ukamilifu hali inayoongeza morali kwa watumishi wa Ofisi hiyo.
“Tangu nimehamia hapa nimeshuhudia kwa kiwango kikubwa kwamba maoni tunayotoa kupitia baraza la wafanyakazi yanazingatiwa hivyo ni jambo la kujivunia na tunapongeza kwa hatua hii” Alisisitiza
Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu linafanyika mjini Dodoma leo Machi 21, 2018 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa uliowekwa na Serikali kupitia Wizara, Mikoa, Wilaya, Idara, Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma kuwapa nafasi watumishi kutoa maoni yao kupitia baraza la wafanyakazi ili kuongeza tija na uwajibikaji katika Taasisi husika.
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.
![]() |
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano leo mjini Dodoma kabla ya kufunguliwa kwa Kikao cha baraza hilo .
|
![]() |
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Flora Bilauri akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
|
![]() |
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Ernajoyce Hallo akiuliza swali wakati wa mkutano wa baraza hilo lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
|
![]() |
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Packshard Mkongwa akiwasilisha mada ya Bajeti ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2018/19 wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo
|
![]() |
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Alex Ndimbo akiuliza swali wakati wa mkutano wa baraza hilo lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
|
Tuesday, March 20, 2018
SERIKALI YATEKELEZA MAOMBI 5 YA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WILAYANI LONGIDO
WAZIRI MKUU AMKABIDHI MSAADA BIBI TACLA HAMIDU (MLEMAVU)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes). |
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.