Chama cha wahandishi wa habari
wanawake Tanzania (TAMWA) kimetakiwa kuweka mkazo mkubwa katika uhuru wa
kujieleza unaojumuisha sauti za wanawake ndani ya ajenda ya jumla ya haki za
binadamu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati
alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu
Hassan katika maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha waandishi wa habari wanawake
Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri, ametoa wito kwa (TAMWA)
kuona umuhimu wa mijadala yenye mlengo wa kijinsia na uhusiano kati ya uhuru wa
vyombo vya habari, ulinzi na usalama wa waandishi wa Habari wanawake, na uhuru
wa kujieleza kuwa kitovu cha kufanya maamuzi katika ngazi ya jamii kitaifa, na kimataifa.
“Tuadhimishe siku hii kutimiza
ahadi zilizotolewa na kila Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuyafikia
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yote na hasa lengo namba tano
linalozungumzia usawa wa jinsia,” alihimiza.
Aidha wadau mbalimbali wa
habari watumie siku hii kusherehekea kwa kuungana na TAMWA kulinda na kuthamini
haki za wanawake, haki za wasichana, haki za watoto, maadili ya kitanzania, na
kupinga ukatili wa jinsia majumbani, hadharani na mitandaoni.
“Wamiliki wa vyombo vya Habari
na waandishi wote kwa ujumla muungane katika jitihada za ulinzi na usalama wa
waandishi wa Habari wanawake na hapa niwatie moyo waandishi wa Habari wanawake
kuwa kazi yenu nzuri inaonekana pale mnapoweka jitihada ya kufanya kazi kwa
weledi bila kukatishwa tamaa na vikwazo vya kimazingira.”Alifafanua
Waziri amesema kama kauli mbiu
inavyosema, Uongozi Bora na Mchango wa Wanawake ni Chachu Kuelekea Tanzania
yenye Maendeleo endelevu.
Hatuna budi kutambua kwamba suala
la jinsia sio suala la wanawake peke yao bali ni suala la kuchochea maendeleo
ya taifa letu miongoni mwa wanawake na wanaume, kwani ni jambo linalohimiza
ushirikishwaji na ujumuishi usioacha kundi lolote nyuma.
Kwa upande wake Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari Bw, Selestine
Gervas Kakele amesema inatambua Mchango wa (TAMWA) na wakati wote serikali
itaendelea kuangalia ujumbe ambao TAMWA na asasi nyingine inatoa.
Tumepokea utafiti kuhusu
unyanyasaji wa kijinsia: (TAMWA) kupitia utafiti huu imesaidia kuvunja ukimya,
matokeo ya utafiti hayalengi kunyoosha
kidole kwa mtu, bali kushirikiana ili tuweze kuishinda vita hiyo.
“Tusimamie weledi na nidhamu
ya kazi na pale vitendo hivi vinapojitokeza: wahanga wasikae kimya jitokezeni,
pazeni sauti na serikali itasikia,” alifafanua.
Awali Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Bi, Joyce Shebe amemshukuru
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko.
“Tumeona jinsi serikali ambavyo
inapitia mifumo ya kisera na kisheria ilikuja na mipango inayopimika katika
kuhakikisha ushirikishwaji na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na masuala
yanayohusu usawa wa kijinsia inatatekelezeka” alibainisha
(TAMWA) tunaahidi kumuunga
mkono kivitendo kwa sababu ni jukumu ambalo tumealianza tangu miaka 36 iliyopita